NGWEA ALA KICHAPO TOKA KWA CHIDI BENZ...!!!

Habari zilizo tufikia ni kwamba msanii wa Hip Hop bongo Chidi Benz, amempiga Cow Bama aka Ngwea nje ya Ambassador Lounge ikiyoko Mkapa tower, posta, usiku wa kuamkia leo. Ugomvi huo ulitokea baada ya Chidi kumzingua Dully alipokua akiingia, ambapo mwisho wake aliamua kuondoka.

Baada ya Dully kuondoka, Ngwea aliamua kumuuliza Chidi (ambae mara nyingi huitana Dogo lao), inakuaje unamzingua kubwa lao, ndipo Chidi alipopaniki na kuanza kutoa lugha chafu huku akitaka kutokumsikiliza Ngwea, inasemekana Ngwea aliamua kukaa kimya lakini Chidi aliendelea kungea kwa hasaira na kusema "ndio nimemzingua kwani yeye nani" na kumbadilikia Ngwea ambae pia aliamua kuachana nae na kurudi ndani kwenye meza aliyokua amekaa na washkaji zake.

Haikuishia hapo Chidi amkamfata kwenye meza hiyo na kuanza kumuongelea mbaya Ngwea, na ndipo Ngwea akaamua kushuka chini ya jengo kwa nia ya kuondoka.

Habari zinaendela kusema akiwa huko huko chini Chidi alimfata na kumpiga, ikiwa ni pamoja na kumkata na chupa mkononi, na kupelekwa hospitali ambapo alitibiwa.

Ngwea alipotafutwa na kuulizwa sababu ya kupigwa kwake  na Chidi anasema haoni chochote kilichomfanya kupigwa na msanii huyo.

Ngwea kwa sasa yupo katika kituo cha polisi Oystabay kwa ajili ya kumfungua mashtaka, licha ya kuumizwa pia ni kutokana na vitisho alivyopewa na Benzi.

Sio mara ya kwanza kwa Chidi kupiga wasanii wenzake, kama unakumbuka alishawahi kumpiga Matonya na wengine kadhaa.

Chidi anaendelea kutafutwa ili aelezea upande wake. Habari kamili sikiliza 255 ya Clouds Fm kesho kuanzia saa saba mchana kupitia kipindi cha XXL.

Source: DJ Fetty

Comments

  1. Kartel is ever killin it. His music is of high grade

    ReplyDelete
  2. Ngwea ulikiwa na vibao vikali hadi leo

    ReplyDelete

Post a Comment