VODACOM NA NOKIA ZAZINDUA NOKIA LUMIA 820 NA 920.

Mkuu wa kitengo cha vifaa vya mawasiliano na wateja wa Vodacom Tanzania Mgopelinyi kiwanga wa Kwanza kushoto, Meneja wa vifaa vya mawasiliano wa Vodacom Elihuruma Ngowi (Katikati) na Meneja Masoko wa Nokia Ellen Lupilli, Wakionyesha kwa waandishi wa habari hawapo pichani. Simu mpya aina ya Nokia Lumia 820 na 920 ambazo kwa mara ya kwanza zimeingizwa sokoni kwa Ushirikiano kati ya Vodacom na Nokia.
Vodacom Tanzania Head of Devices and Acquisition, Mgopelinyi Kiwanga (left) Manager for Alternative Products and Devices Elihuruma Ngowi (centre) and Nokia Tanzania Marketing Manager, Ellen Lupilli show the latest Nokia Phones, Nokia Lumia 820 and 920, which have been launched in partnership between the two companies. Customers are getting1GB free internet for 30 days upon purchase of the phones.
Meneja Mkuu wa Nokia Tanzania Samson Majwala, akiwa pamoja na wafanyakazi wa Vodacom na Nokia katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa simu ya Nokia Lumia 820 na 920 ambazo kwa mara ya kwanza zimeingizwa katika soko la Tanzania.
Baadhi ya Wanyange wakiweka pozi na Simu mpya ya Nokia Lumia 820 na 920 ambayo kwa Mara ya Kwanza imeingizwa katika soko la Tanzania.
Kuhusu Vodacom Tanzania:

Kampuni ya Vodacom Tanzania Limited ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na jamii katika shughuli za maendeleo kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation. Vodacom Foundation ina nguzo kuu tatu: Afya, Elimu na Ustawi wa Jamii. Hadi sasa taasisi hiyo imechangia zaidi ya miradi 120 ya kijamii nchini. Aidha, imeshinda tuzo mbalimbali za kitaifa na za kimataifa katika nyanja ya Uwajibikaji wa Mashirika kwa Jamii. Hizi ni pamoja na East African CSR Awards na Diversion and Inclusion Award ambayo hutolewa na kampuni mama ya Vodafone.

Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania inayotumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano. Vodacom Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South Afritca, ambayo pia ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) Limited inamiliki hisa ailimia 65 Vodacom Tanzania na asilimia 35 zilizobaki zinammilikiwa na Mirambo Ltd.

Vodacom Tanzania imetangazwa kuwa Super Brand (Chapa Bora Zaidi) kwa miaka mitatu mfululizo, kutoka 2009 -2011.
Dar es Salaam, Watuamiaji wa simu za mkononi kuanzia sasa wataanza kunufaika na simu za Nokia Lumia 920 na Lumia 820 zinazokidhi matakwa ya mtumiaji kulingana na teknolojia ya sasa, baada ya Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom nchini kwa kushirikiana na Nokia kuzitambulisha rasmi sokoni.
Simu hizo ambazo zina uwezo wa kuhimili kimatumizi masafa ya teknolojia ya kiwango cha juu yaani 'Long Term Evolution' LTE, zimezinduliwa Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya Vodacom kukamilisha mchakato wa ufungaji minara yake ya 3G nchi nzima na ile ya 4G kwa jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano na Wateja wa Vodacom, Mgopelinyi Kiwanga, alisema kampuni yake inaona fahari na umuhimu kuwaleta karibu wateja wa simu hizo bora (smartphones) katika soko la Tanzania.

"Simu hizi zina uwezo wa kipekee kukidhi mahitaji halisi ya teknolojia ya kiwango cha juu kabisa, ikizingatiwa ubora wake katika kila kifurushi cha huduma yake, mwonekano mzuri wa filamu na picha, haiunganishwi na waya wowote, udadavuaji rahisi wa vifurushi ikiwemo Intaneti, Facebook, Youtube, Twitter, Wikipedia na ina kadi ya kumbukumbu yenye uwezo wa GB 32 na 1GB RAM," alisema Kiwanga.

Aliongeza kuwa kitu kingine kinachokufanya uitambue kwa urahisi Nokia Lumia 920 ni rangi zake ikiwemo manjano, nyekundu na nyeusi wakati Nokia Lumia 820 ina rangi nyekundu, manjano, kijivu, zambarau, nyeusi, nyeupe na sayani.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Nokia Afrika Mashariki, Ellen Lupilli, alisema uwezo wa simu hizo ukilinganisha na smartphones nyingine ina mwonekano safi wa filamu, mafaili na picha, na kutokana na ubora wa lenzi yake unaweza kuchukua picha bila ya kutumia flash usiku na mchana.
Kwa mujibu wa Lupilli, wateja wanaweza kudadavua programu na michezo mbalimbali kama Fifa 12, Tertis na Need for Speed.

"Nokia Lumia 920 na 820 zina vitu vingi vizuri na rahisi kutumia, kiasi kwamba zitawavutia watumiaji wengi kuzinunua," alisema na kuongeza "simu hizo ziko sokoni tayari na unaweza kupata kwenye maduka ya Vodacom nay a Nokia nchini,huku gharama za Lumia 920 ni Sh 1,154,999 na ile ya Lumia 820 inauzwa kwa Sh 809,999," alisema Lupilli.

Comments