Afisa Muuguzi wa Kituo cha Afya cha 'Town' mkoani Lindi, Assumpta Mpiri, akimtoa damu mtoto mchanga kupitia kisigino, tayari kwa kuikausha na kuipeleka maabara kuu ya Taifa ya Muhimbili kwa njia ya mashine 'sms printer' ambayo pia katika kipindi kifupi inauwezo wa kupokea majibu ya vipimo hivyo tayari kwa kumkabidhi mzazi wa mtoto huyo. Mashine hizo takribani 8 zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani elfu 11, zimetolewa mkoani humo kwa msaada wa Vodacom Foundation chini ya uratibu wa Taasisi inayojishughulisha na Mpango wa Tafiti zinazohusiana na Afya ya Uzazi ya EGPAF |
Afisa Muuguzi wa Kituo cha Afya cha 'Town' mkoani Lindi, Faida Ibrahim, kwa kushirikiana na Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon, akimtoa damu mtoto mchanga kupitia kisigino, tayari kwa kuikausha na kuipeleka maabara kuu ya Taifa ya Muhimbili kwa njia ya mashine ya kisasa 'sms printer' ambayo pia katika kipindi kifupi inauwezo wa kupokea majibu ya vipimo hivyo tayari kwa kumkabidhi mzazi. Mashine hizo takribani 8 zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani elfu 11, zimetolewa mkoani humo na Vodacom Foundation, chini ya uratibu wa Taasisi inayojishughulisha na Mpango wa Tafiti zinazohusiana na Afya ya Uzazi ya EGPAF |
Mtaalamu wa Maabara ya Hospitali ya Mkoa wa Lindi, Julius Mwansimba, (kulia) akimuonesha Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon, ufanisi wa mashine 'sms printers' zinazowezesha upatikanaji wa haraka wa majibu ya vipimo vya VVU kwa watoto wachanga ndani ya maabara ya hospitali hiyo jana. Vodacom Foundation chini ya uratibu wa Taasisi inayojishughulisha na Tafiti za Afya ya Uzazi wa mtoto, baba na mama ya EGPAF hivi karibuni ilitoa msaada wa mashine hizo zipatazo 8 mkoani Lindi, zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani elfu 10 |
Afisa Muuguzi wa Hospitali ya mkoa wa Lindi, Zainab Mathradas, (kulia), akimkabidhi mmoja wa wadau wa huduma za afya, ambaye ni Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon, taarifa ya takwimu na matokeo ya ufanisi wa huduma ya Afya ya Uzazi wa mtoto, baba na mama mkoani Lindi. Wengine wanaoshuhudia ni Maafisa waandamizi kutoka Taasisi inayojishughulisha na Mpango wa Tafiti zinazohusiana na Afya ya Uzazi ya EGPAF. Vodacom Foundation hivi karibuni ilichangia mashine 8 'sms printers' zenye gharama ya zaidi ya Dola Marekani elfu 10 mkoani Lindi, zinazowezesha upatikanaji wa haraka wa majibu ya vipimo vya VVU kwa watoto wachanga. |
Mkazi wa Matokeni mkoani Lindi, ambaye anaishi na Virusi vya Ukimwi, Iman Bakari, akiwaeleza wanahabari, na maofisa kutoka Vodacom Foundation na Taasisi inayojishughulisha na Afya ya uzazi wa mtoto, baba na mama ya EGPAF, namna mashine za kisasa 'sms printers'zilivyomuwezesha kupata majibu ya vipimo vya VVU vya watoto wake wawili kwa urahisi na haraka. Mashine hizo takribani 8 zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani elfu 10, zimetolewa mkoani humo na Vodacom Foundation, chini ya uratibu wa Taasisi inayojishughulisha na Mpango wa Tafiti zinazohusiana na Afya ya Uzazi ya EGPAF . |
Mganga Mkuu wa mkoa wa Lindi, Dk Sonda Shaaban, akifafanua jambo mbele ya maofisa wa Vodacom Foundation na Taasisi inayojishughulisha na tafiti zinazohusiana na Afya ya Uzazi ya EGPAF, (hawapo pichani), sanjari na kutoa tathmini ya jinsi mkoa huo ulivyojipanga kukabiliana na changamoto ya afya ya Uzazi wa mtoto, baba, na mama kwenye eneo la maambukizi mapya ya VVU toka kwa baba na mama kwenda kwa mtoto. Vodacom Foundation hivi karibuni ilichangia mashine 8 za kisasa 'SMS PRINTER' zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani elfu 10 ndani ya mkoa huo, katika kuwezesha upatikanaji wa haraka wa majibu ya vipimo vya VVU kwa watoto wachanga. |
Comments
Post a Comment