TAMTHILIA: SIRI YA MTUNGI SEHEMU YA 12 { EPISODE 12 }.

Cheche anapata mkataba wa kufurahisha wa kupiga video ya muziki wa Bongo Flava. Ni kazi anayoifanya kwa mara ya kwanza. Lakini pale anapomsahau Shoti kwenye baa moja ya barabarani, Mwanaidi anaanza kupoteza uvumilivu wake kwa mkwewe mzembe.
Ni mwanzo mpya kwa Stephen katika shule nyingine. Duma anaanza kuelewa kwamba anawajibika kumtunza mdogo wake na hali kadhalika yeye mwenyewe.
Farida yumo kwenye njama ya kumfanyia ufidhuli Nusura na mimba yake. Lakini mapambano yake yanaposhindikana, anamwendea kinyume Kizito na kuelekea kwa Mgongo, mganga wa kienyeji, na kwa Furaha, fundi cherehani mmbeya.

Comments

  1. Hi Jestina,
    Mimi ni mfuatliaji mzuri sana wa tamthilia hii kwenye link yako. Hivi huyu kijana mwenye duka la nguo ni shoga au? Kwani Tanzania ushoga umeruhusiwa? Naona anaigiza kama shoga hii inafundisha nini kwa jamii yetu? Hawa wafadhili wanaingiza huu utamaduni kisiasa sana sababu kwao unakubalika. Watoto wetu wanajifunza nini kwa huyu kijana. Sijapenda huyu kijana alivyoigiza.

    ReplyDelete

Post a Comment