BREAKING NEWS: ALBERT MANGWEA AFARIKI DUNIA NCHINI AFRIKA KUSINI.

Taarifa zilizozotufia sasa hivi zinaeleza msanii maarufu wa muziki wa hip hop, Albert Mangwea amefariki dunia.
Habari kutoka kwa mtu wa karibu na Rapper Ngwea, aliejitambulisha kwa jina la Hamisi, amesema Ngwea alikua kule kwa mualiko wa kufanya show South Africa, ambapo alikua na msanii mwingine anaeitwa M to the P, na walitakiwa kuondoka leo kurudi Dar saa tatu asubuhi, lakini baada ya kuona hawatokei ndio wakaamua kwenda walipokuwa wamefikia na kuwakuta wote wawili wakiwa hawajielewi baada ya kujidunga madawa ya kulevya mengi (overdose), walipowahishwa hospitali, habari ndio ikawa hivi, kuwa Ngwea amefariki na M to the P yuko hoi katika hospitali ya St hellen iliyo jijini Johannesburg, Afrika Kusini. 
Bado tunaendelea kufuatilia kujua kuhusiana na hali halisi ya tukio hilo linalomhusu msanii huyo aliyeanza kutamba na songi la Ghetho Langu na Mikasi.
"Mungu Amlaze mahali pema peponni Ameen"



Comments