MANCHESTER CITY WAMFUKUZA KAZI MENEJA WAO "ROBERTO MANCINI".


Manchester City manager amefukuzwa kazi ikiwa ni mwaka mmoja sasa tangu timu yake ilipochukuwa ubingwa wa England "Premier League".
Mtaliana huyo yamemkuta hayo baada ya timu yake kutofanya kama ilivyofikiriwa na wenye club hiyo na kumaliza msimu wa ligi mikono mitupu.

Taarifa ya mtandao wa  club hiyo ulisema kwa masikitiko makubwa tunatangaza kuwa Roberto Mancini ameondolewa kwenye umeneja wa timu hiyo.

"Haya yamekuwa ni maamuzi magumu kwa mwenyekiti mmiliki, na bodi kufanya na ni matokeo ya mwisho yaliyofikiwa baada ya mchakato wa majadiliano baina ya pande zote mbili.


 Mwenyekiti wa klabu hiyo Khaldoon Al Mubarak alisema: rekodi ya  Roberto inaonekana na kila mtu  na kwamba kwa niaba ya Sheikh Mansour, pamoja na yeye mwenyewe pamoja na wafanyakazi wote wanamtakia mafanikio mema huko aendako .



Comments