OIKO CREDIT KUONGEZA MIKOPO KWENYE KILIMO NA NISHATI ENDELEVU.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya OIKO Credit Duniani  David Woods  akiongea na waandish wa habari  (hawapo pichani) kuhusiana na Taasisi y a oiko kuongeza mikopo kwenye sekita ya Kilimo na nishati endelevu  hapa nchini  wakati alipotembelea katika ofisi za Oiko Credit zilizopo   jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Mkurugenzi wa  Oiko Kanda ya Afrika Mashariki  Judy Ngarachu na kulia ni  Meneja wa taasisi hiyo hapa Tanzania Deus Manyeynye.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya OIKO Credit Duniani  David Woods akimkabidhi  Devota Elias fedha ambaye ni mmoja wa wanachama wa kikundi cha Aple ambacho kimenufaika na mikopo ya  shilingi million 8  toka kwa taasisi ya Oika Credit ,anaye shuhudia katikati ni Meneja wa taasisi hiyo hapa Tanzania Deus Manyeynye. Mkurugenzi huyo yopo katika ziara ya kikazi hapa nchini kujionea jisi shughuli za taasisi hiyo inavyoendeshwa.
Mkurugenzi wa  Oiko Kanda ya Afrika Mashariki  Judy Ngarachu  akimkabidhi fedha Jane Mlay   ambaye ni mmoja wa wanachama wa kikundi cha Aple ambacho kimenufaika na mkopo ya  shilingi million 8  toka kwa taasisi ya Oika Credit  nchini  katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya OIKO Credit Duniani  David Woods, Mkurugenzi Mtendaji wa Tujenge Tanzania Limited Shafi Nambobi   na Meneja wa taasisi hiyo hapa Tanzania Deus Manyeynye. Mkurugenzi huyo yopo hapa nchini kwa ziara ya kikazi hapa  kujionea jisi shughuli za taasisi hiyo zinavyoendeshwa.
---
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
OIKO CREDIT KUONGEZA MIKOPO KWENYE KILIMO NA NISHATI ENDELEVU
Dar es Salaam 9, May, 2013.. TAASISI ya OIKO Credit inayojihusisha na utoaji mikopo kwa taasisi mbali mbali za fedha duniani, imewahidi kuongeza mikopo katika sekta za kilimo pamoja na nishati endelevu hapa nchini.Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo David Woods aliyeitembelea Tanzania hivi karibuni na kukutana na baadhi ya wateja alisema “Mikopo yetu kwa Afrika inalenga zaidi kwenye kilimo, vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa (SACCOS) vimekuwa vikitoa mchango mkubwa kufanikisha lengo hili. Pamoja na kilimo hapa Tanzania tunaangalia eneo lingine ambalo ni nishati endelevu, nafurahi kuwepo Tanzania na kuendeleza ushirikiano wetu wa muda mrefu.

Taasisi ya Oikocredit ambayo pia hutoa mikopo na mitaji kwa taasisi za kilimo pamoja na biashara ndogo na za kati (SMEs)  ilifungua ofisi zake hapa Tanzania mwaka 2006 na tayari imeshatoa mikopo yenye thamani ya shilingi 15bn/- kwa miradi 35 hapa nchini

Ikiwa ni moja kati ya vyanzo vikubwa duniani binafsi vya kutoa mitaji kwa mifuko midogo (microfinance), ufadhili wa taasisi hiyo kwa miradi mbalimbali duniani umekuwa na kufikia Tshs 1.1 trilioni (Euro 530 milioni) mwaka 2012 ongezeko la asilimia 2 kutoka 1. 07 Trilioni (Euro milioni 520) mwaka 2011. Secta ndogo (microfinance) inawakilisha karibu asilimia 79 ya mikopo ya taasisi hiyo. Ya pili ni kilimo na usindikaji ambayo huchukua asilimia 12 ikifutiwa na biashara ambayo ni asilimia 3 na elimu na afya vikichukua asilimia 3 pia.

Kilimo kinaendelea kuwa moja ya sekta muhimu kwa Oiko credit na kwa sasa ina imarisha dirisha la mikopo ya kilimo. Oikocredit tayari imehidhinisha 51.2BN/-(Euro milioni 25) katika mikopo mipya 38 kwa wabia wake wa kilimo kwa mwaka 2012 na kutoa kiasi cha 72bn/-(Euro milioni 35) kwa sekta ya kilimo kwa ujumla. Baadhi ya uwekezaji unagharamia ununuzi au ujenzi unahusisha majengo, vifaa vya kilimo na shughuliza za uongezaji wa thamani katika mazao ya kilimo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Mashariki wa taasisi hiyo Judy Ngarachu alisema “Katika nchi za Kenya na Tanzania kumekuwa na ari ya kuendeleza miradi ya nishati endelevu, lakini jamii zimekuwa zikihangaika kutafuta wawekezaji binafsi kuwasaidia kupitia upembuzi yakinifu, mipango pamoja na maandalizi. Naamini tunaweza kutoa mchango muhimu katika miradi kama hii,”

Meneja wa Oikocrediti kwa Tanzania Deus Manyenye alielezea umuhimu wa kilimo na kusema, “Kilimo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania. Kilimo kinachangia nusu ya pato la taifa, robo tatu ya bidhaa zinazosafirishwa nje na pia ni chanzo cha chakula. Inatoa ajira kwa asilimia 80 ya watanzania, wanawake wakiwa ndiyo nguvu kazi muhimu katika sekta hii. Tunafurahi kutoa mchango wetu katika kampeni ya kilimo Kwanza iliyozinduliwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2009.

Comments