Siku ya Jumamosi 27.04.2013 Watanzania Wanaoishi Ujerumani , chini ya mwamvuli wa umoja wao (UTU) Waliuhakikishia ulimwengu kuwa neno "MUUNGANO" lina maana
kamili kwa maisha ya mtanzania na binadamu wengine.
Sherehe hizo zilizowakusanya watanzania na marafiki wa Tazania kutoka kila kona ya ujerumani, ziliutingisha mji wa koloni katika Usiku usio kwisha wa kusherehekea miaka 49 ya muungano wa Tanzania.
Mhe.Ali Siwa naibu balozi wa Tanzania nchini Ujerumani alikua mstari wa mbele akiwaongoza watanzania katika Muungano Day,
Wasanii mbali mbali walitumbuiza jukwaani na kuipeperusha vilivyo bendera ya Tazania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania ujerumani Mh.Mfundo na kamati yake wameahidi
kufanya mambo makubwa na kuitangaza Tanzania kwa hali na mali chini ya Umoja wa watanzania Ujerumani(UTU)
Mh.Ali Siwa wa Ubalozi wa TZ Berlin,akizungumza na Mzee.Katabalo (mtumishi mstaafu wa UN )
Mh.Ali Siwa,mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania,Berlin akitoa hotuba ya Ufunguzi
Mhe.Ali Siwa akiwa Msanii John Gambula kutoka Bagamoyo.
Dada Nashe Mvungi akionyesha bidhaa za Tanzania kwa wageni.
Msanii Dada Joanita Henry(Mwenyeji wa muungano Day Koloni) akiwa na msanii mwenziwe kutoka Zimbabwe.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Shah Smooth akiwarusha wageni.
Muungano oyeeee! huyu dogo naye ndani ya nyumba.
Msanii John Gambula na Tadeo Simon, wakiwa na watoto jukwaani.
Wageni mbali mbali wakiipongeza Tanzania, mwenyekiti wa UTU Mh. Mfundo aliyevaa shati la kitenge akiongoza shughuli.j
wageni wakijichagulia Bidhaa za Tanzania.
Wasanii wa kikundi cha Wabantu group wakiipeperusha TZ.
Wasanii wa kitanzania wakiepeperusha TZ katika maigizo n.k
Comments
Post a Comment