Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria halfa hiyo ya kuwawezesha wateja wa kampuni ya GNLD kuanza kulipia bidhaa mbalimbali zenye ubora wa kimataifa kupitia huduma ya M-Pesa. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wateja GNLD sasa kulipia bidhaa kwa njia ya M-Pesa Dar es Salaam, Mei 6, 2013 ... WATEJA wa huduma ya M-Pesa nchini sasa watanufaika na huduma hiyo ya teknolojia ya simu kwa kuwawezesha watanzania kwa mara ya kwanza kulipia bidhaa za kampuni ya GNLD Tanzania inayouza dawa asilia zenye ubora wa kimataifa kupitia huduma hiyo ya M-Pesa.
Huduma ya M-Pesa, imeendelea kurahisisha maisha ya watanzania kwa kupanua huduma zake katika sekta mbalimbali za kibenki wakati huu ikishuhudia kuingia katika ushirikiano kati ya Kampuni ya Vodacom Tanzania na Kampuni inayohusika na uuzaji wa dawa asilia zenye ubora wa kimataifa ya GNLD Tanzania. Mpango huu umelenga kunufaisha wateja kwa kuweza kulipia bidhaa za GNLD kwa njia ya huduma hiyo ya M-Pesa.
Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa, wateja ambao wako tayari kulipa kwa ajili ya bidhaa za GNLD hawana sababu tena ya kubeba fedha kwa sababu za usalama.
"M-Pesa ni huduma ambayo ni salama na ya haraka. Kutokana na ushirikiano huu, wateja hawatakuwa na sababu ya kupoteza muda wao kwenda kwa wakala wa GNLD kulipa kwa ajili ya bidhaa fulani. Wanachotakiwa kufanya ni kutumia huduma ya Vodacom M-Pesa na kufanya malipo," anasema Mtingwa.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa GNLD Tanzania, Daniel Mutiso, anasema kwamba GNLD itaendelea kuhakikisha kwamba inaendelea kutoa huduma yenye kiwango cha juu cha ubora ili kukuza afya bora kwa kila mtu.
"Ushirikiano huu ni wa kwanza na wa aina yake katika soko hili. Hivyo tunajisikia furaha kufanya uzinduzi huu leo kwasababu utaweza kusaidia kila mtu katika nchi hii," anasema Mutiso.
Kulipia bidhaa za GNLD kupitia huduma ya M-Pesa, wateja watakiwa kupiga *150*00# na kuchagua Malipo na kisha kuingiza namba ya Biashara ambayo ni 000221na kufuatiwa na namba ya akaunti ikifuatiwa na Kiasi kisha Namba ya Siri (PIN) na mwisho kufanya uthibitisho.
Comments
Post a Comment