BREAKING NEWS: MSANII WA HIP HOP TANZANIA LANGA AFARIKI DUNIA.

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba msanii Langa afariki dunia..
Langa Kileo (msanii wa Hip Hop Tanzania, pichani) amefariki dunia leo
Langa alipelekwa hospitali akiwa hajitambui. Anadaiwa kuwa alikumbwa na Malaria kali sana, Hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili jana.
Uchunguzi wa chanzo cha kifo chake bado unaendelea.Msanii Langa aliwahi kutamba na kikundi cha Wakilisha pamoja na witness na sara ni miongoni mwa wasanii wakongwe wa bongo flava nchini Tanzania.Mungu amrehemu, Ameen

Update:
Langa Mengisen Kileo, leo jioni amefariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar baada ya kuugua malaria na kisha kujitokeza homa ya uti wa mgongo.

Akizungumza na matandao huu, baba mzazi wa Langa, Mzee Mengesen Kileo, amesema alimpeleka mwanaye Hospitali ya Kinondoni maarufu ‘Kwa Dokta Mvungi’ ambapo aligundulika kuwa na malaria na baadaye aligundulika kuwa na homa ya uti wa mgongo. Mzee Mengisen aliongeza kuwa, baada ya Dokta Mvungi kugundua kuwa Langa ana homa ya uti wa mgongo ambayo ni hatari, leo asubuhi aliamua kumkimbiza hospitali ya Muhimbili na kumfikishia chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU’. 

Baba huyo wa marehemu alizidi kuueleza mtandao huu kuwa, ilipofika mida ya saa kumi jioni, mwanaye aliaga dunia. Mipango ya mazishi inaendelea kupangwa nyumbani kwao marehemu Mtaa wa Chato, Mikochocheni jijini Dar. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. 

Comments

  1. oooops wots goin' on wth our Artists
    .. May His soul Rest in peace

    ReplyDelete
  2. r.i.p langa we love u broo
    mpe hai brother ngwea mwambie wa bongo bado twamlilia.oooooohhhhhh god who is next.help us dear god we stil need our artist .

    ReplyDelete

Post a Comment