MREMBO aliyejulikana kwa jina la Pepetua Maina au maarufu kama Lucy, Mkikuyu wa Kenya anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mpaka 30 amekutwa amekufa kwa kuchinjwa shingo na mwili wake kutupwa katika shimo la taka. Mwili huo ulikutwa na polisi Juni 8, mwaka huu Mikocheni B, jirani kabisa na makazi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.
Mwili wa Pepetua baada ya kufunikwa. |
Taarifa za kipolisi zilidai kuwa mrembo huyo kabla ya kuchinjwa alipigwa kwani mkono mmoja wa kushoto ulivunjika na kukutwa na jeraha kubwa katika paji la uso.
Mwili wa Pepetua ukitolewa shimoni na polisi. |
Juni 9, mwaka huu, mwandishi alizungumza na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Camillius Wambura kuhusu kifo cha msichana huyo ambapo alikiri kutokea.
Mwili wa Pepetua baada ya kutolewa shimoni. |
Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari. |
“Tuliuchukua na kwenda kuuhifadhi Hospitali ya Mwananyamala. Vijana wawili wanaoishi kwa Jaji Kileo ndiyo waliofika hospitali na kumtambua marehemu. Jaji mwenyewe alikuwa safarini nje ya nchi, amerejea leo (juzi Jumapili).
“Mpaka sasa tunamshikilia mtu mmoja kwa mahojiano kuhusiana na kifo hicho, siwezi kuzungumza kwa undani zaidi,” alisema Afande Wambura.
Comments
Post a Comment