MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA WAONDOKA KUELEKEA MOROGORO.

 Jeneza lenye mwili wa Albert Mangwea likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya Morogoro ambako ndo atazikwa.
 Mapaprazii wakichukua picha za mwisho mwisho
 Gari likianza safari yake kuelekea Morogoro
Hapa ni Miembe 7 karibu na Mlandizi Pwani, hawa ni baadhi ya mashabiki wa marehemu Ngwea waliojitokeza barabarani kuuaga mwili wa marehemu. Wakati huo huo wananchi wa maeneo ya mikese, wamekusanyika na kuusimamisha msafara uliobeba mwili wa marehem Ngwea kwa kutaka na wao wamuage, akizungumza na Cloud Fm "Moe Fire" amesema walikutana na kundi la watu na kudhani labda kuna tatizo. Baada ya kusimamishwa na trafic na kuuliza tatizo ni nini, Trafic alisema kuwa wananchi hao wamekusanyika ili kuuaga mwili wa marehem Ngwea na kudai kitendo hicho kikifanyika ndio amani itapatikana.
Kilichofanyika ni kuruhusu watu wale walishike gari lililokuwa na mwili wa Ngwea na kuondoka, lakini baada ya kuondoka, zaidi ya pikipiki 50 walizozikuta pale ziliongoza msafara huku magari mengine pia yakiunga msafara huo.
Sehemu ya umati mkubwa wa watu wajitokeza kupokea mwili wa Albert Mangwea Morogoro


Masanja mkandamizaji akiwa na Zola D nyumbani kwa Mama Albert Mangwea Morogoro 
 Mwili wa marehemu Mangwea ukiingia nyumbani kwao Morogoro
 Watu walikuwa ni wengi sana hadi juu ya miti walipanda
Baada ya kufika nyumbani mwili ukapelekwa kuhifadhiwa mochwari. Kesho taratibu zote za safari yake ya mwisho zitafikia ukingoni.

Comments