 |
Msomaji wa Quran tukufu katika mashindano ya kitaifa, Abdallah Abdulkadri akisoma wakati wa fainali zake leo
|
 |
Msomaji wa Quran tukufu katika mashindano ya kitaifa, Seif Salim Said ambaye ni mremavu wa macho akisoma wakati wa fainali zake leo
|
 |
Baadhi ya viongoza wa Dini wakifatilia mashindano hayo leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee |
 |
Baadhi ya wanafunzi walioshiliki katika kusoma Quran tukufu |
 |
Msomaji wa Quran tukufu katika mashindano ya kitaifa, Ummy Swaleh Said ambaye ni mremavu wa macho akisoma wakati wa fainali zake leo
|
 |
Baadhi ya waumini wa Dini Ya Kislam wakiongozwa na Bi,Aisha Sururu wakifatilia Mashindano Hayo |
Bi Aisha Sururu akifatilia mashindano hayo yaliyomalizika leo
 |
Zawadi walizopewa washindi |
Mgeni Rasmi wa Mashindano ya kuifadhi Quran tukufu kitaifa DR, Suleiman Ally Yussuf katikati na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran ,Morteza Sabouri wakimkabizi zawadi wa chereani mshindi wa kusoma juzuu 20
 |
Mgeni Rasmi wa Mashindano ya kuifadhi Quran tukufu kitaifa DR, Suleiman Ally Yussuf kulia akimkabidhi mshindi bajaji na pesa taslimu laki tano mshindi Abdul Hamid |
|
 |
Baadhi ya washindi wa kuhifadhi Quran Tukufu wakiomba Duwa baada ya kumalizika mashindano hayo |
|
Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya kitaifa ya kuhifadhi Quran tukufu yamemalizika leo, huku walemavu wa viungo wakiwa kivutio cha aina yake, kwa kuonyesha maajabu.
Walioshangiliwa na hata kuwatoa machozi watazamaji walikuwa ni Ummy Kuluthumu Swaleh Saidi kutoka Pemba, ambaye hakuwa na miguu wala mikono pamoja na Seif Salim Said ambaye ni mlemavu wa kuona na kusikia, waliweza kusoma vizuri bila kubabaika huku wakiwapita hata wale waliokuwa na viungo kamili.
Mashindano hayo yalimalizika jana Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo yalihusisha washiriki 72 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Walemavu hao pamoja na wengine sita, walizawadiwa fedha taslim pamoja na fimbo za kuwawezesha kutembea.
Nafasi ya mshindi wa kwanza kwa wavulana ilikwenda kwa Abdul Hamid na msichana alikuwa Suria Ally Bakari ambao kwa pamoja walipewa Bajaji na fedha taslim sh. 500,000.
Washindi wa mashindano hayo yaliyoandaliwa na Eshe Sururu Foundation, yaligawanywa katika makundi matano, kwa upande wanawake na wanaume, huku washindi wengine wakiondoka na pikipiki, baiskeli, vyereheni na fedha taslim.
Katibu wa kamati ya maandalizi, Issah Ramadhan Mohamed alisema kuwa madhumuni ya kuandaa mashindano hayo ni kuibua ari kwa vijana wa kiislam waweze kusoma Quran Tukufu kwa mustakabali wa maisha mema.
Alisema yalishirikisha wasichana 38 na wavulana 34 ambapo kila upande alitoka mshindi wa kwanza hadi wa tatu na yaligawanywa kwa ngazi tano ikiwemo kuhifadhi Juzuu 20,10, tano na tatu.
|
Comments
Post a Comment