Wananchi wakibeba mwili wa marehemu baada ya kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana. |
Mwanaume mmoja ambaye hakujulikana jina lake mara moja, muda mfupi uliopita ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wauaji ni wanaume wawili waliokuwa katika pikipiki maarufu kama 'Bodaboda'. Marehemu alikuwa akishuka katika gari lake aina ya Toyota Mark II yenye namba za usajili T 508 ADY ndipo alipopigwa risasi kadhaa. KWA HABARI ZAIDI NA PICHA ZA TUKIO HILI, tutazidi kuwafahamisha.
Chanzo: Global Publishers
Kusema ukwlei matendo ya uhalifu yanaendela kuongezeka Tanzania je hali hii itaendela mpaka lini? Tatizo hasa ni umaskini kweli au tu ni uzoefu. Inasikitsha sana. R.I.P
Kipindi hiki cha kuelekea siku kuu ya Eid el Fitr tutaona matukio mengi ya kihalifu. Ni kazi ya wana usalama kujipanga tu kwani si rahisi kujua ni wapi, lini na muda gani nini kitatokea!
ReplyDelete