NDIKUMANA (MME WA IRENE UWOYA) NDANI YA MOVIE NA LUCY KOMBA.

Muigizaji maarufu Lucy Komba amemsifia Hamad Ndikumana (Kataut) ambaye ameigiza nae katika filamu mpya ya "Kwanini Nisimuoe" kuwa ana kipaji cha uigizaji tofauti na alivyofikiria mwanzoni kuwa inaweza kuwa shida kidogo wakati alipomfuata kwa ajili ya utengenezaji wa filamu hiyo. Ndikumana ni msakata kambumbu maarufu akiwa mwenyeji wa Rwanda na alimuoa muigizaji maarufu nchini Irene Uwoya miaka michache iliyopita ingawa kwasasa wanadaiwa kutengana. 

Akichonga na mwandishi wa habari hizi kutokea nchini Denmark, Lucy Komba alisema "Ndiku ana kipaji kusema ukweli wakati namchukua kufanya nae kazi nilijua nitapata nae tabu sana lakini ni tofauti na nilivyofikiria ni mtu mmoja kichwa sana yaani msanii ni msanii tu alicheza mpaka mwenyewe nilifurahi kwa kifupi ana kipaji cha uigizaji, maelekezo kweli nilimpa na kumfundisha nilimfundisha lakini uchezaji wake ulikuwa juu zaidi"

Lucy Komba ameibua waigizaji wengi maarufu wanaotamba sasa wakiwemo Jackline Wolper, Mzee Chillo na Irene Uwoya hivyo usije kushangaa Ndiku akifanya kweli kwenye kiwanda cha filamu. Filamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni muda sio mrefu.           

Source: Swahili World Palent


Movie coming soon stay tuned

Comments