Penny akimlisha cake mama mkwe wake aka Mama Naseed na baada ya tukio hili Diamond Platnumz amefunguka na kuandika yafuatayo kupitia blog yake: "Hadi sasa nashindwa kuelewa lakini ntaelewa tu......ni mapenzi ya dhati juu ya mama yangu mzazi..... Siku ya jana ilikuwa siku njema kwangu na kwenye maisha yangu,ni siku ambayo mama yangu mzazi amezaliwa 7.7....
Kutokana na majukumu na kazi kuingiliana nilishindwa kufanya chochote kama mnavyojua nilikuwa na kibarua kizito kinanisubiri uwanja wa taifa kwenye tamasha la matumaini so nsingweza kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja..... Lakini chakushangaza kabisa nimewasili usiku na crew yangu natokea kwenye show nikakuta nimeachiwa kipande cha keki sikuelewa imetoka wapi kwa kuwa mihadi yangu na mama yangu ilikuwa ni Jumatatu ya leo kumpeleka kula chakula cha jioni kusherekea siku yake hiyo kutokana na majukumu ya kazi kuingiliana.... Nilichostajabishwa ni hiki na kufurahishwa sana mpaka kufikia machozi kunilenga ni pale nilipokutana na picha hizi na kuziangalia..... Kiukweli nilikuwa sijui chochote na hadi hapa navyoandika naona kama ndoto.... Nimejaribu kumuuliza mama yangu nae anasema akutambua kama kingekuwa kitu hiko laasha alipigiwa simu kwenda kwa mazungumzo ya biashara kati yake na Peniel na ghafla kukuta familia na marafiki wakimsubiri wakiongozwa na PENIEL MUNGIRWA aliyefanya usiku wa mama yangu kuwa wa furaha kabisa.... Shukrani za zati kwake kwa moyo wa ukarimu na mwenyezi mungu azidi kumzidshia na amfanyie wepesi wa kila jambo lake la kheri...... Nami nikaona nisishuudie pekee yangu basi na wewe shabiki yangu tuangalie wote kilichojiri pale Protea hotel,masaki jijini Dar es salaam.....!!" |
Comments
Post a Comment