TAARIFA YA MSIBA JAJI (MSTAAFU) BUXTON DAVID CHIPETA.

MAREHEMU JAJI (MSTAAFU) BUXTON DAVID CHIPETA.

Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na
Wafanyakazi wote wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(SUMATRA), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA anasikitika kuufahamisha umma kuwa
aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SUMATRA Jaji (Mstaafu)
Buxton David Chipeta amefariki dunia tarehe 16 Julai, 2013 katika Hospitali ya
Hindu Mandal, Dar es Salaam.


Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Marehemu,
Oysterbay Mtaa wa Chole/Lincon, Plot No. 580.


Tunaomba tuungane na Familia ya Marehemu Jaji (Mstaafu)
Chipeta katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya msiba huu mkubwa.


Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina Lake
Lihimidiwe!


 The London Family inatoa pole kwa familia ya marehemu.  Mungu awe pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu. May dad's soul R.I.P


Comments