MFANYABIASHARA ERASTO MSUYA WA JIJI LA ARUSHA AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NN

WADAU KUMRADHI KWA PICHA HIZI KAMA ZITAKUKWAZWA.

Mwili wa Marehemu Erasto Msuya ukiwa umelala mita chache karibu na gari lake aina ya Vogue. 
Pichani askari Polisi wakiwa eneo la tukio kwa ajili ya kuubeba mwili wa Marehemu ERASTO MSUYA. 
 Mwili wa Marehemu ERASTO MSUYA ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Boma n’gombe ukiwa na majereha pamoja na matundu ya risasi kifuani.

 Mfanyabiashara maarufu wa madini na mmiliki wa hoteli ya SG RESORT na MEZZALUNA mkoani Arusha Milionea ERASTO MSUYA ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana mchana huu eneo la KIA akitokea Mererani kuelekea Moshi.

Polisi wanaendelea na uchunguzi baada ya kuuchukua mwili wa marehemu kutoka kwenye eneo la tukio na kuupeleka hospitalini. Mwili wa marehemu upo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Bomang’ombe.

JG Blog itaendelea kukupa updates juu ya tukio hili.

Comments