KESHO NDO KESHO NDANI YA MJI WA READING.

Katibu wa CHADEMA kanda ya Kaskazini MH. A Golugwa na Balozi wa Tanzania hapa UK MH. P Kalaghe leo mchana wamekutana ofisini kwa balozi. Pamoja na mambo mengine, walizungumzia shughuli nzito ya kesho - Operesheni Komboa Tanzania 2015 : BBQ Funga Mwaka itakayofanyika mji wa Reading kesho kuanzia saa sita mchana.  Watanzania wote karibuni kwa wingi. Nyama choma, viburudisho na mambo mengine mengi.



Comments