Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, siku ya Ijumaa 18 Octoba 2013 uliwaaga rasmi maofisa wake wawili ambao wameteuliwa rasmi na Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. MHE. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kuiwakilisha nchi katika nafasi tofauti. Maofisa hao wa kwanza ni Mheshimiwa Balozi Chabaka Kilumanga, ambaye alikuwa Naibu Balozi katika Ubalozi huo wa Tanzania - London, ambaye hivi sasa ameteuliwa na Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano, Tanzania kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Comoro.
Ofisa mwingine ambaye ameagwa rasmi katika sherehe hiyo fupi iliyofanyika Ubalozini hapo ni Bwana Syslevster Ambokile, ambaye nae pia ameteuliwa na Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, kabla ya kuteuliwa kwake Bwana S. Ambokile alikuwa msaidizi wa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Tanzania.
Kwenye picha ya pamoja na Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe (kulia), Mama Joyce Kallaghe (Kushoto), Wafanyakazi wa Ubalozi, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye sherehe hiyo ya kuwaaga rasmi. |
Comments
Post a Comment