Mawakala wa M-pesa nchi nzima wameendelea kujishindia zawadi za fedha taslimu kupitia promosheni ya Mkwanja Kwa Wakala inayoendeshwa na Vodacom kwa shabaha ya kuwawezesha mawakala wake hao kuwa na sababu nyengine ya kufurahia kuwa sehemu ya mafanikio makubwa ya huduma ya M-pesa hapa nchini.
Zaidi ya mawakala wa M-pesa 1,350 kutoka mikoa yote wameshajishindia zaidi ya Sh. 135 Milioni katika promosheni hiyo iliyobakisha wiki tatu kufikia ukomo wake baadae mwezi ujao.
“Promosheni inakwenda vizuri na kikubwa zaidi mawakala wetu wameipokea na kuifurahia sana, hili ndilo haswa lililokuwa lengo letu.”Alisema Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim
Mwalim aliongeza kuwa “Tunawatembelea washindi wote popote pale walipo iwe mjini au kijijini na kukaa nao na kupitia kwao wanatupatia mawazo mengi mazuri ya namna ya kuboresha huduma yetu hii ambayo kwa sasa imekuwa mkombozi mkubwa kwenye maisha ya watanzania.”
M-pesa ina mawakala zaidi ya 55,000 nchi nzima na kuwa huduma pekee ya miamala kwa njia ya simu za mkononi yenye mtandao mkubwa zaidi wa mawakala na hivyo kuwa huduma inayoongoza kwa kufikiwa kwa urahisi na kwa ukaribu zaidi na watanzania mijini na vijijini.
Ili wakala wa M-pesa aweze kuingia kwenye droo ya kila wiki anapaswa kuwa amefanya miamala isiyopungua mitano kwa siku. Mawaka 270 hujishindia Sh 100,000 kila mmoja kwenye droo hizo zinazosimamiwa na bodi ya michezo ya kubahatisha.
Kupitia M-pesa mteja wa Vodacom anaweza kufanya miamala na zaidi ya biashara 350 ikiwemo kununua tikiti za ndege, kulipia ada, kutoa au kuweka fedha kwenye akaunti ya benki za biashara zaidi ya 15, kulipia kodi TRA, kununua muda wa maongezi wa hewani, kulipia huduma za ving’amuzi vya televisheni, kununua luku, kulipia huduma za maji n.k.
Comments
Post a Comment