Bwana, Ramadhani Juma (Katikati) Mkazi wa Nane Nane Morogoro, akipokea hundi ya shilingi laki 100000, kutoka kwa Meneja wa Vodacom kanda ya kati Nguvu Masapila, baada ya kujishindia kutoka katika Promosheni ya Mkwanja kwa Wakala yenye lengo la kuboresha maisha ya mawakala wa kampuni ya Vodacom. Hadi sasa kampuni hiyo imetoa fedha taslimu kiasi cha shilingi Milioni 81 na vyetri kwa mawakala 810 wa M-pesa nchini ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini Mchango wao kwa jamii ya watanzania na kampuni hiyo. Pamoja nao katika picha ni Mkaguzi wa Mawakala Ahmed Kaunda. |
Comments
Post a Comment