TAARIFA YA MWALIKO KUTOKA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA.

UBALOZI WA TANZANIA LONDON
Simu:  020 7569 1470                                                                                                                       3 Stratford Place,
Fax: 020 7491 3710                                                                                                                             London W1C 1AS
Barua pepe: balozi@tanzania-online.gov.uk
Mtandao: www.tanzania-online.gov.uk        

KAMATI YA KUDUMU YA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA YA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI UINGEREZA


Kamati ya kudumu ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , ikiongozwa na Mwenyekiti wake Dkt Hamisi Kigwangalla (Mb), ipo nchini Uingereza kwa mwaliko rasmi wa Bunge la Uingereza.



Kamati imependezwa kutumia fursa ya ziara hii kusikia mawazo ya watanzania waishio nchini Uingereza kuhusu masuala yanayogusa maslahi yao ya kimaendeleo na nchi yao kwa ujumla.

Kwa niaba ya Kamati ya Kudumu ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Ubalozi wa Tanzania London unapenda kuwaalika watanzania waishio nchini Uingereza katika ofisi za Ubalozi siku ya Ijumaa tarehe 29 Novemba 2013 kuanzia saa 11.00 jioni kushiriki mkutano na kamati hiyo.

Watanzania wote mnakaribishwa.

Ubalozi wa Tanzania
London-UK

Comments