WASHIRIKI WAWILI WA MISS TANZANIA USA PAGEANT WALALAMIKIA MATOKEA NA KUDAI HAYAKUWA YA HAKI [AUDIO].

Julia Nyerere
Hellena Nyerere
Washiriki wa Miss Tanzania USA Pageant wana ndugu wawili, Julia Nyerere na Hellena Nyerere  wamepost malalamiko yao kuhusu uchaguzi wa washindi kupitia kurasa zao za facebook na kusema mashindano hayo hayakuwa ya haki kwani wanaamini walistahili kuwemo kwenye nafasi za mshindi wa kwanza hadi wa tatu na kukejeli kwa kuiita Miss Bukoba USA Pageant,  blog ya Vijimambo ilimpigia simu Julia Nyerere ili kujua undani kuhusu madai yake hayo ambayao yamerekodiwa hapa chini. Sikiliza kwa makini
Hawa ndio waliokuwa majaji katika shindano hilo kutoka kushoto ni Miss Sierra Leone, Peter Walden na aliyekuwa Miss District Of Columbia 2012. Blog ya Vijimambo ilitaka kujuwa ukweli juu ya tuhuma hizi na iliongea na jaji Mtanzania aliyekuwa mmoja wa majai usiku huo, Peter Walden na haya ndio aliyosema.
Vijimambo bado inaendelea na juhudi za kumtafuta mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Tanzania USA Pageant Ma Winny Casey tusikie upande wake.

Stay tuned the saga continues.........

Comments