Meneja wa Vodacom kanda ya Kusini, Henry Tzamburakis akikabidhi msaada wa chakula kwa kituo cha wa watoto yatima cha EAGT Rahaleo Manispaa ya Mtwara Mikindani. Wanaopokea msaada huo kutoka (kushoto) ni watoto wanaoishi katika mazingira magumu Yasunta Rawland, Boniface Seleman, Mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto cha EAGT Mtwara, Caroline Mkwele, Askofu wa kanisa la EAGT Rahaleo Mtwara pia (mwasisi wa kituo) George Mrope. Vodacom kanda ya kusini inatarajia kutumia Tsh.Milioni 3 kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali katika jamii ya kanda ya kusini. |
Comments
Post a Comment