DODOMA FM 98.4 | NEWS | JAN 27,2014
TAKRIBANI WATU 583 WAMEATHIRIKA NA MAFURIKO YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KATIKA KATA YA MPUNGUZI MKOANI DODOMA NA KUSABABISHA NYUMBA 146 KUANGUKA .
Akizungumza na Dodoma fm Diwani wa kata ya mpunguzi mh john Matonya ameseama pamoja na idadi hiyo ya nyumba zilizo anguka bado nyingine zinaendelea kuanguka .
Aidha mh matonya amesema miundombinu mibovu ndio chanzo cha mafuriko hayo kutokana na kujengwa bila kiwango kizuri.
Hata hivyo mh matonya ameomba miundombinu iboreshwe ili kuondoa adha ya mafuriko wakati mvua zinaponyesha.
WAMILIKI WA MITANDAO YA SIMU ZA MKONONI TANZANIA WAMEELEZA SABABU ZINAZOPELEKEA WAO KUSHINDWA KUWEKA MINARA YA SIMU KATIKA MAENEO YA VIJIJINI
Hayo yamejiri mara baada ya wakazi wa kijiji cha solowu wilayani chamwino kulalamikia ukosefu wa mawasiliano ya mitandao ya simu kwa muda mrefu .
Akizungumza na Dodoma fm Mfanyakazi wa mtandao wa zantel Bw Brayan Donard amesema ukosefu wa miundombinu vijijini ndo sababu kubwa inayowapelekea wao kushindwa kuwafikia wakazi wa maeneo hayo.
Aidha Bwana Brayani ameongezea kuwa wana malengo ya kuwafika watanzania wote ila kwa sasa wameanza na wakazi wa Dodoma mjini na wanaelekea vijijini.
Sanjari na hayo amewataka wakazi wa maeneo ambayo yamekuwa yana matatizo ya mtandao wawe wavumilivu kwani wanawakumbuka na muda ukifika watawafikia
DIWANI WA KATA YA CHILONWA WILAYANI CHAMWINO AMEITAKA SERIKALI KUJENGA DARAJA LA CHILONWA LILILOSABABISHA WATU WATATU KUPOTEZA MAISHA KUFUATIA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.
Akizungumza na Dodoma fm Mh Yaledi Sinon amesema tangu kutokea kwa tukio hilo mpaka sasa hakuna harakati zinazofanyika baada ya meneja wa mkoa kuahidi kutafuta jitihada za matengenezo.
Aidha mh Sinoni amesema tangu kutokea tukio hilo mpaka hivi sasa hakuna kiongozi yeyote aliefika hapo kwa ajili ya kutatua kero hiyo.
Hata hivyo ameomba madereva kuwa makini katika daraja hilo kutokana na kuendelea kunyesha kwa mvua na kuwataka makandarasi kutengeneza daraja hilo.
ZAIDI YA MAGARI 1,000 YAMEKWAMA KWENYE BARABARA KUU YA MWANZA KWENDA DAR ES SALAAM KATIKA KATA YA MIGUWA, WILAYANI NZEGA, KUTOKANA UTEKAJI WA MALORI ULIOFANYWA HIVI KARIBUNI.
Madereva wamegoma kuondoa magari yao baada ya kukasirishwa na kitendo cha polisi wa Nzega kushindwa kuwasaidia wakati walipotekwa.
Kutokana na tukio hilo,madereva wamegoma kuondoa magari yao na kusababisha mabasi ya abiria na malori ya mizigo kukwama wakati abiria wapatao 3,000 wakitaabika kwa kukosa chakula na maji.
Aidha Madereva hao wameapa kutoondoa magari hayo hadi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa watakapofika kwenye eneo hilo ili kusikiliza kilio chao.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nzega, Emmanuel Mihayo amesema watu wamejeruhiwa vibaya kwenye utekaji huo kwa kukatwa masikio na kutobolewa macho.
WATU WANNE WAMEPOTEZA MAISHA KWA KUSOMBWA NA MAJI MKOANI HAPA , KUTOKANA NA MVUA ZINAZO ENDELEA KUNYESHA NCHINI.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime amesema watu hao wanatoka maeneo tofauti lakini vifo vyao vimetokea kwenye mito inayotiririsha maji kwa msimu.
Katika tukio la hivi karibuni mkazi mmoja wa kijiji cha Mpinga mwenye umri wa miaka 55 amefariki baada ya kutumbukia kwenye mto Mpinga ambao ni wa msimu.
Kamanda Misime amesema tukio jingine limetokea mwanzoni mwa wiki iliyopita, ambapo watu wanne walitumbukia na gari waliyokuwa wakisafiria katika mto Chinyasungwi, kijiji cha Mahampa, Wilayani Chamwino na watatu kati yao walikufa huku mmoja akiokolewa.
HABARI ZA KIMATAIFA
DAMASCUS
MAZUNGUMZO YA AMANI KUHUSU SYRIA YANAYOENDELEA MJINI GENEVA YANATARAJIWA KUINGIA SIKU YA NNE HIVI LEO ILI KUJARIBU KUYAJIBU MASWALI YA KISIASA YANAYO ULIZWA IKIWEMO SWALI LINALO HUSIANA NA KUKABIDHI MADARAKA.
Akizungumza katika mkutano huo Naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Syria Faisal Mikdad amesema kuwa serikali ya Syria iko tayari kuwaruhusu watoto pamoja na wanawake kuondoka na Serikali ipo tayari kuwapokea na kuwapa misaada ya madawa, makao na mahitaji mengine ya msingi .
Mpatanishi wa umoja wa mataifa Lakhdar Brahimi amesema hatua hiyo ya kwanza ni muhimu katika mazungumzo hayo ingawa hapakuwa na makubaliano kuhusu swala la kuachiliwa huru kwa mahabusu,
Mazungumzo ya leo yataangazia pia maswala ambayo hayajapata suluhu kama vile kuruhusu misafara ya magari yanayobeba misaada ya chakula kuingia maeneo yaliyozingirwa na majeshi ya serikali katika mji wa kale wa Homs.
TRIPOLI
WANADIPLOMASIA WATANO WA MISRI WALIOTEKWA NYARA IJUMAA ILIYOPITA MJINI TRIPOLI, NCHINI LIBYA WAMEACHIWA HURU.
Ripoti iliyotolewa na kituo cha televisheni cha al-Arabiya imesema, mateka hao walipelekwa kwenye wizara ya mambo ya ndani ya Libya ambapo Mtekaji mmoja ameiambia televisheni hiyo kwa njia ya simu kuwa wamefikia makubaliano na serikali ya Misri,kuhusu kumwachia huru kiongozi wao baada ya wanadiplomasia hao kuachiwa huru.
Wanadiplomasia hao kutoka ubalozi wa Misri nchini Libya walitekwa usiku wa Ijumaa iliyopita saa kadhaa baada ya kukamatwa kwa El-Zawy, kiongozi wa kundi moja la kijeshi na polisi wa Misri. Baada ya utekaji huo kutokea, Misri iliwaita wafanyakazi wote kwenye ubalozi wake nchini Libya.
NEW YORK
KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA BAN KI-MOON AMEPONGEZA KUPITISHWA KWA KATIBA MPYA NCHINI TUNISIA NA KUSEMA HIYO NI HATUA KUBWA YA KIHISTORIA NCHINI HUMO.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu huyo imesema, Ban Ki moon amefurahia majadiliano na upatanishi wa kitaifa uliosababisha mabadiliko ya mpito wa kidemokrasia nchini Tunisia, na kufanikisha kupatikana kwa katiba mpya nchini humo.
Aidha amesema hatua iliyopigwa na Tunisia ni mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine yanayotaka kufanya mageuzi na ametoa wito kwa wahusika wa kisiasa nchini Tunisia kuhakikisha kuwa hatua hiyo inafuata mpito wa kisiasa nchini humo.
ADDIS ABABA
VIONGOZI 54 WA AFRIKA WANATARAJIWA KUKUTANA WIKI IJAYO MJINI ADDIS ABABA, ETHIOPIA ILI KUJADILI MASUALA YA KILIMO NA USALAMA WA CHAKULA BARANI AFRIKA.
Mkutano huo unatarajia kufanyika siku ya Alhamisi na Ijumaa wiki hii wenye huku kauli mbiu yake ikiwa ni "Kubadilisha Kilimo cha Afrika kwa ajili ya kuhimiza ukuaji na Maendeleo Endelevu",katika mkutano huo viongozi watajadili changamoto za kilimo ikiwemo kupungua kwa rutuba ,mabadiliko ya hali ya hewa
viongozi wa Afrika watatafuta njia za kufufua sekta ya kilimo ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Afrika. Viongozi hao watajadili changamoto za kilimo ikiwemo kupungua kwa rutuba, mabadiliko ya hali ya hewa, upungufu wa maji na ardhi ya kilimo.
Kwa muda mrefu, Afrika imekuwa ikitilia mkazo umuhimu wa kilimo katika kupunguza umaskini na kuhimiza ukuaji wa uchumi.
|
Comments
Post a Comment