Mpiga tumba maarufu wa bendi ya muziki wa dansi, Twanga Pepeta, Soud Mohamed ‘MCD’ aliyefariki jana usiku, atazikwa kesho majira ya saa saba mchana, mjini Moshi.
Kwa mujibu wa kiongozi wa bendi hiyo, Luiza Mbutu, familia ya marehemu MCD imekubali kusogeza mbele muda wa mazishi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo majira ya saa kumi ili kuwapa nafasi ndugu jamaa na marafiki walioko mbali kuweza kuhudhuria mazishi hayo.
Wajumbe wa Kamati itakayoratibu safari ya kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi na kusaidia katika taratibu za mazishi wamechaguliwa jana usiku, na wajumbe waliochaguliwa ni Omar Baraka (Mkurugenzi msaidizi ASET), Hassan Rehani (Meneja ASET), Abdallah Dossi (Mwenyekiti Macamp ya ASET), Martin Sospeter (Meneja Mashujaa Musica), Taasis Masela (Kiongozi Akudo Impact), Deo Mutta (Katibu wa Macamp ya ASET), Rehema Kiluvia (Mdau Twanga Pepeta), Super Nyamwela (Kiongozi Mkuu Shoo Extra Bongo), na Muweka hazina ni kiongozi mkuu wa Twanga Pepeta Luizer Mbutu.
Michango ya kusaidia mazishi inapokelewa na mweka hazina kupitia namba zake za simu ambazo ni 0653 797976, 0762 460090 na 0787 090090.
HAKIKA MCD UMEENZIWA
Shukrani nyingi kwa wadau wa Muziki wa Dansi kwa kuweka tofauti pembeni na kushiriki kwa asilimia mia kuhakikisha suala la kuwezesha watu kwenda Moshi usiku huu. Ahsante kwa michango kutoka kwa bendi zifuatazo;
1. Mapacha Watatu
2.FM Accademia
3. Mashujaa Musica
4. Acudo Impact
5. Extra Bongo
6. Malaika Band
7. Kalunde Band
8. Bongo Movie na
9. Mtandao wa Wanamuziki chini ya Mzee Kitime.
Michango yenu imewezesha safari ya Moshi iliyoanza saa tano na nusu usiku huu. Ahsanteni sana.
Comments
Post a Comment