MOTO MKUBWA WAUNGUZA JENGO LA RK BARABARA YA NYERERE DAR.

Jengo la RK lililokaribu na eneo la Jet katika Barabara ya Nyerere karibu na sheli ya Victoria linaendelea kuwaka moto mkubwa mchana huu ambao umefika katika eneo la ghala la kuhifadhia madawa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wapo eneo la tukio ambako hali bado si shwari.
Sehemu iliyoathirika zaidi  ni ghala la kutunzia dawa za binadamu la kampuni ya Phillips.
Moto bado ni mkubwa na unaendelea kuteketeza mali katika jengo la RK lililopo Jet Barabara ya Nyerere japo vikosi mbalimbali vya Zimamoto vipo vikiendelea kujaribu kuzuia moto huo. Magari yenye maji yanazidi kuongezwa eneo la tukio ambapo watu ni wengi wanaoshuhudia tukio hilo.
Mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kupoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo.
 (HABARI:HARUNI SANCHAWA/GPL , PICHA NA MDAU SHUMBUSHO)

Comments