
Mmiliki wa Blog ya Chahangamoto yetu, Mubelwa Bandio mwenye makaazi yake DMV mapema leo alitembelea kaburi la mwanamuziki wa reggae aliyewika enzi hizo marehemu Jastin Kalikawe ambaye pia alikua mdogo wake marehemu Dj Kalikali huko Bukoba na kupata nafasi ya kufanya mahojiano na mjane wa marehemu Bi.Georgia na binti yao Abayo mara alipowatembelewa nyumbani kwao Bukoba alipoenda maalum kwa likizo ya kikazi.

Mmiliki wa Blog ya Chahangamoto Yetu, Mubelwa Bandio mwenye makaazi yake DMV nchini Marekani na mtangazaji wa Jamii Production akifanya mahojiano na majane wa marehemu Justin Kalikawe Bi. Georgia nyumbani kwao Bukoba mara tu alipowasili Bukoba kwa likizo ya kikazi.

Kaka Mubelwa Bandio akifanya mahojiano na mtoto wa marehemu Justin Kalikawe Abayo nyumbani kwao Bukoba mara tu alipowasili Bukoba kwa likizo ya kikazi.

Mubelwa Bandio katika picha ya pamoja na mama na mwana.
Mubelwa akiwa katika mahojiano na Burhan Bushako mpwa wa Hayati Justin Kalikawe ambaye ameeleza mengi kuhusu mjomba wake!
Mubelwa akiwa anamfanyia mahojiano Arnold Kalikawe kikazi anajulikana kama Ras Nold mtoto wa Kaka wa Hayati Justin Kalikawe
Mubelwa akiwa katika picha ya pamoja na Arnold Kalikawe kikazi anajulikana kama Ras Nold mtoto wa Kaka wa Hayati Justin Kalikawe mara baada ya mahojiano
Mubelwa akiwa na watoto wa ndugu zake Justin Kalikawe aliyeachia Rasta ni Burhan Bushako. mtoto wa dada ya Justin na mwenzake ni Ras Nold. Mtoto wa kaka wa Justin
RASTAs wa Bukoba nao walikuwa na la kusema kuhusu Justin Kalikawe
Hii ni kazi moja wapo ya marehemu Justin Kalikawe
Comments
Post a Comment