![]() |
Watu takribani 500 walilala hapa Jangwani bus station. Hadi sasa hakuna chakula. — Irenei Kiria Aprili 13, 2014. |
Ikiwa unataka kusaidia walioathirika kwa mafuriko ya mvua jijini Dar es Salaam, tafadhali soma mahitaji yaliyoorodheshwa hapo chini kisha wasiliana na wahusika ili kuwasilisha mchango wako wa hali na mali:
Wale mnaotumia Twitter, tafadhali search, trend #DarFloods kwa taarifa zaidi.
Uncle Fafi @Tanganyikan anasema: "Michango itaanza kupokelewa saa saba mchana na tutaongeza vituo kadiri itakavyowezekana. Vituo vya msaada" ni hivi vifuatavyo:-
- Sayansi (COSTECH) - @Mcshady41
- Kinondoni Leaders Club - @Tanganyikan
- Ilala - @AbbyKirahi (money sent to 0767003322, Abraham Donald Kirahi)
- Survey - @RebecaGyumi
- Sayansi - @McShady41
- Temeke - Piga 0713484896
- Kwa Kigamboni unaweza kuacha mchango wako FAT supermarket iko Maweni, mwachie muuzaji.
Unaweza kuchangia: Vyakula, sabuni, maji, nguo, mashuka, magodoro, vyandarua, mahema na kwa wakina mama/dada kama una kanga, pedi n.k.
Kwa ambaye unapenda kuchangia fedha taslimu tafadhali tumia namba: 0767003322, 0763516506
Kwa utakayeamua kuchangia fedha taslimu tafadhali sema unataka zinunuliwe kitu gani.
Tofauti na 2011, mwaka huu hakuna vituo vya kuelekeweka kwa waathirika. Wahanga wamehamia jirani ambako maji hayajafika.Kwa eneo ulilopo tafadhali muulize mjumbe wa mtaa/balozi kuna watu wangapi wanahitaji msaada. Wengi wamehamia kwa majirani.Tumepita kwa mjumbe mmoja maeneo ya msasani, amezihifadhi familia 3 na katuonyesha kaya nyingine zilipojihifadhi kwa majirani zao
Tumekutana na @AbbyKirahi @iEdwn @MissiePopular @rickyboshe @McShady41 na@martheritta tunajiandaa kwenda fire kukutana na @WaljiAli
HIZI NDIYO NUMBER PEKEE ZA KUTUMA MCHANGO WAKO HAKUNA NYINGINE. CHANGIA SASA 0767003322, 0763516506 #DarFloods #DarFloods
Comments
Post a Comment