USIKU WA OLD IS GOLD REGENCY JUMAPILI HII APRIL 20 2014.

Pichani ni Mwanahawa Ally  na Rukia Ramadhan

Na Andrew Chale

WAPENZI wa nyimbo za zamani za taarabu asilia nchini, jumapili hii ya Aprili 20, ya Pasaka..wanatarajiwa kupata burudani safi na zawadi nyingi zitakazotolewa na Fabak Fashion ndani ya ukumbi wa  Regency Hotel, Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, miongoni mwa wadhamini wa onesho hilo, amewaomba wadau kujitokeza kwa wingi kufurahia usiku huo kwa kukumbushiana enzi sambamba na zawadi lukuki zitakazotolewa kwa njia ya bahati nasibu.
Asia Idarous alisema onesho hilo la kila Jumapili,  usiku huo wa ‘Old is Gold na Spice Modern Taarab,’  pia watafurahia pamoja na wadau katika kusherehekea Pasaka, ambapo  wasanii nguli waalikwa watakuwamo.
“Jumapili hii ndani ya Old is Gold, pia wasanii Mwanahawa Ally na Rukia Ramadhan, watakuwapo kuwasindikiza  Spice Modern taarab, hivyo shamrashamra kuwa kubwa zaidi,” alisema Asia Idarous.
Kuhusu kiingilio, alisema kitakuwa sh 5,000 tu,  watafurahia burudani hiyo ya aina yake zikiwemo nyimbo za mwambao hasa zile zilizokuwa zikipendwa, kuanzia saa 12 jioni hadi saa sita usiku sambamba na kuchezesha bahati nasibu na kugawa zawadi kutoka Fabak Fashion.
Asia Idarous alizitaja baadhi ya nyimbo wanazotamba nazo wasanii  hao waalikwa ni ‘Nikumbatie’ wa Rukia Ramadhan  na ‘Usiku wa Awali’ wa Mwanahawa  Ally.
Wadhamini wengine katika usiku huo wa taarabu asilia ni Times FM, Regency Park Hotel na Fabak Fashions.

Comments