Dar es Salaam umeingia ugonjwa wa homa ya Dengue uking'atwa na mbu hao unaugua na very risk unaweza pona au usipone inamaliza damu na maji mwilini na homa kali sana.
Jitahidini kufunga milango ili hao mbu wasiingie majumbani na uchafu usikae karibu na madimbwi ya maji machafu.
Hatari sana.
Hospital nyingi wameshapokea wagonjwa na hauna kinga zaidi ya kuomba ulinzi kwa Allah na kujilinda mwenyewe na hao mbu.
Wizara ya Afya imetangaza kua makini sana.
HOMA YA DENGUE NI NINI?
Homa ya Dengue ni ugonjwa unaoenezwa kwa kuumwa na mbu aina ya Aedes mwenye virus vya ugonjwa huu. Mbu hupata virusi vya homa ya Dengue anapomuuma mtu mwenye ugonjwa huu.
Ugonjwa huu unaenezwa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine kwa kuumwa na mbu huyu.
DALILI:
Homa kali ya ghafla
Kuumwa kichwa hususani sehemu za machoni
Maumivu makali ya viungo na misuli ya mwili
Kichefuchefu au kutapika
Kutokwa na damu kwenye fizi, na sehemu za uwazi za mwili.
Uchovu
ukimsikia ndugu au jamaa yako anasema kuwa na dalili hizi muwahishe hospitali mapema.
#SAMBAZA KUWASAIDIA NA WENGINE.
Comments
Post a Comment