Jack wa Chuzi akiwa wodi namba 2 wa hospital ya Aghakan Morogoro
Nesi akimuhudumia
Rashid akimuhudumia Jack Wa Chuzi
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MWIGIZAJI Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’ mwishoni mwa wiki iliyopita alizua utata katika Hospitali ya Aghakani ya mkoani hapa baada ya kunaswa akiuguzwa na kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Rashid Said.
Baadhi ya watu waliofika kumtembelea Jack aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Typhoid, walihoji juu ya ukaribu wa Rashid ambaye ni kinyozi mjini hapa na staa huyo ndipo paparazi wetu alipowauliza wawili hao kwa nyakati tofauti, kila mmoja akatoa jibu lake
“Huyu ni shemeji yangu kwa bwana angu ambaye baada ya kupata taarifa za mimi kulazwa alifika hapa toka mwanzo na kunihudumia,” alisema Jack huku Rashid akisema
“Jack ni rafiki yangu na kwamba baada ya mimi kupata taarifa za kuugua kwake, nilikuja kumhudumia.” Jack baada ya kulazwa kwa muda hospitalini hapo, aliruhusiwa na kurejea nyumbani kwake, Dar.
Kwa habari zaidi za Morogoro tembelea Shekidele Blog
People need to get a life! Kisa cha kumfatilia kinyozi na kumuuliza uhusiano wake na Jack ni nini kama sio umbea?
ReplyDelete