Mwenyeji wa mkutano huo Mwinjilisti Jailous Maloda akihu
biri kwenye mkutano huo
Baadhi ya umati wa watu uliofulika kwenye mkutano huo
Masanja mkandamizaji[wapili kutoka kushoto] akifuatilia mahubiri hayo
Wakati wenzake wa meza kuu wakisimama na kufanya maombezi Masanja aliamu kuketi na kuwa bize na simu yake jambo lililowasanja na kuwachefua watu waliofulika kwenye mkutano huo
Akizidi kuwa bize na simu hiyo kama alivyonaswa na kamera za Mtandano huu.
Na Dustan Shekidele, Morogoro.
MCHUNGAJI mtarajiwa ambaye pia ni mwimbaji mahairi wa nyimbo za lnjiri nchini Emmanuel Mgaya'Masanja Mkandamizaji,hivi karibuni aliwachefua waumini wa madhehebu mbali mbali walifulika kwenye mkutano wa lnjiri uliofanyika kwenye viwanja wa shule ya Msingi Kiwanja Cha ndege Mkoani hapa kwa kitendo chake cha kuwa bize na simu wakati muhubiri akiendele kuwalisha watu neno la mungu.
Baadhi ya waumini walimshuhudia Masanja akifanya jambo hilo lisilokubalika kwenye ibada au makongamano yoyote ya kinini waliamu kumtonya paparazi wa habari hizi ambaye alimpiga picha nyingi mchungaji huyo mtarajiwa akiwa bize na simu yake huku watumishi wenzake wakisimama na kushiriki kikamilifu katika maombi hayo.
Haijafahamika mara moja kama Masanja alikuwa bize na kutumia meseji kwenye simu yake au alikuwa bize kuchati na marafiki zake kwenye mitandao ya kijamii.
" Huyu Masanja ni mtumishi wa Mungu inakuwaji wake wa maombezi yeye anachti na simu na marafiki zake tene akiwa madhebahuni,sisi waumini wa kawaida kujifunzi nini kutoka kwake akiwa kama kioo cha jamii'alisema Bi Joyce Evarist kwa jazba
Juhudi za Mtandao huu za kutaka kuzungumza na Masanja kuhusiana na tukio hilo ziligonga mwamba baada ya kuzongwa na watu wengi waliogombe kupiga naye Picha mara baada ya kukamilika kwa mkutano huo ambapo baada ya kupiga picha na watu kadhaa mabausa waliokuwa kwenye mkutano huo walimnyanyua na kumwingiza kwenye gari na kutoweka eneo hilo.
Mchungaji huyo mtarajiwa pia ni mwigizaji na mchekezaji mahiri anayepiga kazi kundi la Original Komedy linalolusha michezo yake kupitia luninga ya taifa TBC.
Source: Shekidele Blog
Comments
Post a Comment