MUHUTASARI WA HABARI ZA KITAIFA NA MATAIFA KWA SIKU YA LEO 2 MAY 2014.

DODOMA

Wadau wa elimu mkoani Dodoma wametakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha wiki ya elimu itakayo  fanyika kitaifa  mkoani  Dodoma.

Akizungumza katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi  Mkuu wa Mkoa Wa Dodoma  Dr Rehema nchimbi amesema  mkoa wa Dodoma ndio mwenyeji wa sherehe hiyo kutokana na kwamba itazinduliwa Kitaifa Mkoani hapa katika viwanja vya jamhuri.

Aidha Dr Nchimbi  amezitaka taasisi zote za elimu kuweka mabanda katika viwanja vya jamuhuri ili kuonyesha utendaji kazi wa taasisi hizo.

Pia amekitaka chama cha walimu CWT kuweka banda katika viwanja hivyo  ili watu wakitambue chama hicho na kuwataka walimu kuwa na mshikamano ili kufanikisha wiki ya elimu kikamilifu.

Maadhimisho ya wiki ya Elimu yanatarajiwa kuanza  tarehe 3Mei mwaka 2014.

----------------------------------------------------------------------------------------------

Wakazi  wa manispaa ya Dodoma wameiomba serikali kuwapunguzia wafanyabiashara kodi ya mapato ili waweze kunufaika na  shughuli wanazofanya .

Wakizungumza na Dodoma fm wakazi hao wame sema ni vema serikali ikawapunguzia wafanyakazi  ulipaji wa kodi  ya mapato ili waweze  kuwa na maisha mazuri.

kwa upande wake Rais  wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  Dr, Jakaya  Mrisho Kikwete  amesema  watalishughulikia suala la ulipaji kodi kwa wafanyakazi kadri ya uwezo wa serikali.

Aidha Rais Kikwete amesema  kwa  sasa wataanzisha mfuko maalum kwa lengo la kuwasaidia wafanyakazi pindi  wanapopatwa na matatizo

--------------------------------------------------------------------------------------------------

Wananchi katika manispaa ya Dodoma wametoa mitazamo  yao kuhusiana na mikutano ya kundi linalo unda katiba ya wananchi (UKAWA) inayo endelea mjini Zanzibar.

Wakizungumza  na kituo hiki wakazi hao wamesema wanaimani na UKAWA kwakuwa katika muungano huo kuna wanasiasa makini ambao wamo katika mioyo ya watanzania na hivyo watanzania wanaamini wataleta mabadiliko.

Naye bw . Merkezedek William mkazi wa Ibihwa amezungumzia suala la umoja huo kutaka kuungana kwenye uchaguzi mkuu ujao ambapo amesema  kwa mujibu wa katiba ya sasa haijasema wazi juu ya vyama vya siasa kuungana au kutokuungana na kuweza kusimamisha mgombea mmoja  katika chaguzi mbalimbali.

Akitoa mtazamo wake mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Bwana Anord Mtajwaa amesema UKAWA ni umoja ambao umeona Tanzania inahitaji  nini ndio maana wamejitoa muhanga kwaajili ya kuwatetea wananchi.

KITAIFA

Wananchi  wametakiwa kujitokeza kwa wingi  kupiga kura ya maoni ili kupata katiba bora itakayokidhi matwakwa ya wananchi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania .

Akizungumza katika  sherehe za uzinduzi wa mbio za mwenge kitaifa zilizofanyika mkoani Kagera makamu wa rais Dr ghalib billaly  ambaye alikuwa  mgeni rasmi katika uzinduzi huo amewataka wananchi kujitokeze katika zoezi la  kupiga kura za maoni ili kupata katiba bora itakayokidhi matakwa ya wananchi.

Naye mkuu wa mkoa huo Kanali   mstaafu Fabia  Masawe amesema kuwa mwenge utakapo kuwa katika mboi zake mkoani humo utaambatana na jumbe mbalimbali kama katiba ni sheria kuu ya nchi jitokeze kupiga  kura ya maoni tupate katiba mpya pamoja na mapambano dhidi ya ukimwi  na dawa za kulevya.

Aidha mkuu huyo wa mkoa ameishukuru wizara ya habari utamaduni na michezo pamoja na wizara ya uwezesha ustawi wa jamii vijana wanawake na watoto  na serikali ya  Zanzibar kwa kuuteua mkoa wa kagera kuwa mwenyeji  wa sherehe hizo.

------------------------------------------------------------------------------------------------

 KIMATAIFA 

Maafisa nchini Nigeria wamesema kuwa watu 19 wameuawa baada ya mlipuko kutokea katika kituo cha basi katika mji mkuu wa Nchi hiyo  Abuja.

Mlipuko huo umetokea katika eneo la Nyanya, karibu na kituo cha basi ambako zaidi ya watu sabini waliuwawa katika shambulizi la tarehe14 mwezi Aprili Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya Ripoti za awali zimesema kuwa watu kadhaa wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Waandishi wanasema kuwa mlipuko huo umesababishwa na bomu lililotegwa ndani ya gari huku mtu mmoja   aliye shuhudia kisa hicho amesema aliona miili 20 ya watu waliouwawa katika tukio hilo.

Hakuna kundi lolote  lililodaiwa  kuhusika  katika  shambulizi hilo lakini kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limewahi kutekeleza mashambulizi kama hayo mjini Abuja

-------------------------------------------------------------------------------------------------

Maafisa nchini Colombia bado wanajaribu kuwanusuru takriban watu thelathini waliozikwa wakiwa hai na mamia ya tani ya tope pamoja na mawe baada ya mgodi haramu wa dhahabu kuporomoka usiku wa jumatano.

Waokoaji wanajaribu kufukua udongo ili kuwanusuru watu waliozikwa na udongo huo ulio lowa chepechepe huku miili mitatu imepatikana.

Takriban mashine saba za kufukua udongo zimekuwa zikihusika katika shughuli ya uokozi katika mgodi huo ulioko kusini magharibi mwa sehemu ya Cauca.

Kando kando mwa mgodi huo wapo mamia ya jamaa na marafiki wa  wachimba migodi waliofukiwa ambao wanafuatilia kwa karibu shughuli za uokoaji.

Ijumaa  ya wiki iliyopita, wachimba migodi wengine wanne walipoteza maisha yao huku sitini na tano wengine wakiathirika na gesi ya sumu katika sehemu ya Antioquia.

-------------------------------------------------------------------------------------------------

Wanaharakati nchini Syria wamesema  jeshi la serikali limetekeleza shambulizi la hewani katika soko moja lilikoko katika sehemu inayothibitiwa na waasi  wa Aleppo.

Shambulizi hilo la hewani lilitekelezwa Kaskazini mwa Syria wilayani Halak katika soko moja kuu ambapo Bomu liliangushwa  kwa kutumia ndege.

Watu thelathini wameripotiwa kuuawa katika soko hilo  huku Picha na video za maiti zilizofunikwa na vifusi na majeruhi zimeonyeshwa katika mitandao ya kijamii ambapo Picha hizo zimeonyesha watu wakikimbia kwa taharuki katika barabara za mji huo.

Wapiganaji  na waasi wameanza upya mashambulizi dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na serilaki ya Rais bashar al Asad.

Comments