MWANAMKE MJAMZITO APIGWA MAWE HADI KUFA KISA KAOLEWA NA MWANAUME ANAEMPENDA HUKO PAKISTAN.

Screen Shot 2014-05-28 at 10.26.15 PM
Mwanamke mmoja ambaye alikuwa na ujauzito nchini Pakistan amepigwa mawe hadi kufa nje ya jengo la mahakama kwa kosa la kuolewa na Mwanaume anayempenda badala ya mwanaume aliyechaguliwa na familia yake.

Kilichomkuta Farzana Parveen mwenye umri wa miaka 25 kinawakumba Wanawake wengi nchini Pakistan na katika nchi nyingine ambapo April 2014 Tume ya haki za binadamu nchini Pakistan ilisema Wanawake 869 nchini humo waliuwawa kwa namna hii nchini Pakistan.
mjamzito
Ferzana aliuwawa kwa madai ya kuiabisha familia yake ambapo mauaji hayo yamefanywa na cha kushangaza zaidi hata ndugu wa familia yake wameshiriki katika tendo hilo la kumuua.

Screen Shot 2014-05-28 at 10.28.41 PM


Comments