NEWS ROUNDUP - MUHUTASARI WA HABARI MAY 28, 2014.

 

NEWS BULLETIN MAY 28

dodomafm@ymail.com

logo
---
banner
---
 DODOMA
Kundi la mbwa wenye kichaa limezuka katika Mtaa wa Swaswa  Manispaa ya Dodoma na kusababisha hali ya taharuki  baada ya kuwangata watu wawili na kuwasasabishia maamuvu makali. 
Akizungumza na kituo hiki mzazi wa  mmoja wa mtoto  alieng’atwa na mbwa hao Bw  Jonathani Ngossi amesema  kuwa mbwa hao wamekuwa wakiwang’ata watu wazima na watoto hivyo kupelekea  kutibiwa kwa gharama kubwa.
Aidha Bw Ngossi imeitaka serikali kwenda kutoa chanjo kwa mbwa hao ili kupunguza  tatizo hilo na kama ikishindikana  iwapige risasi  mbwa hao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa huo Bw Chales Nyuma amekiri kuwepo kwa  tatizo hilo na kusema kuwa mpaka sasa watu wawili pamoja na kuku wawili wameshang’atwa na mbwa hao na wanaendelea kutishia amani mtaani hapo
Sanjari na hayo Bwana Nyuma   ameongezea kuwa  kwa baadae  wanakusudia kutoa elimu  kwa watu wenye mbwa juu ya  taratibu za kuwafuga.

Serikali  kwa kupitia wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa imetangaza shabaha yake kuu ya kuitangaza Tanzania kuwa ni sehemu salama kwa uwekezaji.
Hayo yamesemwa na Waziri wa mambao ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bwana Bernard Membe alipokuwa akitoa hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara yake ambapo amesema kuwa shabaha hiyo itasaidia kutekeleza sera ya diplomasia ya uchumi.
Kwa upande wake msemaji wa Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni Bwana Ezekiel Wenje amesema kwamba Tanzania inatakiwa kutumia balozi zake ili kutumia fursa za kiuchumi katika  kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini
Akichangia hotuba hiyo Bi Mary Mwanjero amesema watanzania wanaotoka katika sekta binafsi  washirikishwe na kuwe na kitengo mahususi cha  diplomasia ya uchumi  ili kuwepo na utekelezaji mzuri wa sera ya diplomasia ya uchumi

Wakazi wa mkoa wa Dodoma wameshauriwa kulima mazao yanayoendana na ardhi ya mkoa wa Dodoma.
Akiongea na makala ya nyakati zinabadilika ya kituo hiki afisa kilimo wa wilaya ya Chamwino Bwana Aithani Chaula amesema kuwa wakulima wanatakiwa kuangalia ardhi yenye rutuba ambayo itaendana na zao husika.
Aidha Bwana Chaula ameongeza kwamba  kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi wakulima Mkoani Dodoma wanashauriwa  kulima mazao yanayoendana na ardhi ya mkoa wa Dodoma hususani  zao la mtama aina ya mesia.
Sanjari na hayo Bwana Chaula amewataka wakulima kutumia wanyama kazi katika shughuli zao za kilimo na kupanda mazao yanayokomaa  mapema ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

KITAIFA
Serikali imewataka wamiliki wakubwa wa leseni za umiliki  wa ardhi kwa ajili ya uchimbaji wa madini kuyaendeleza maeneo hayo ili kuepuka kunyanganywa  nakupatiwa wachimbaji wengine. 
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri  wa Nishati na Madini  Bwana Steven Masele wakati akijibu swali la mbunge wa jimbo la Solwa  lililopo Shinyanga vijijini  Ahmed  Aly Salumu  lililohoji juu ya utoaji wa leseni  kwa wachimbaji wadogo wamadini.
Aidha Bwana  Masele amesema kuwa wizara hiyo inaendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo kuhusu umuhimu wa kuwa na leseni na kuwasisitiza wachimbaji wakubwa kuwaachia  wachimbaji wadogo baadhi ya maeneo ambayo wachimbaji hao wanachimba kwa wingi.
Pia amesema kuwa  umiliki wa ardhi kwa hati za kimila hautoshi kutoa haki ya kuchimba madini hivyo kupitia  wizara wanahamasisha wachimbaji wadogo kuomba leseni ili wapate haki ya kuchimba madini.

 KIMATAIFA .
Wagonjwa wapatao 20 pamoja na muuguzi  mmoja wamefariki  huku wengine sita wakiwa mahututi baada ya moto mkubwa kuwaka hospitalini  nchini Korea Kusini.
Inasemekana kwamba Wengi wa walioaga dunia  ni wazee wanaokadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 70 na 80 na wasioweza kutembea ambapo Maafisa wamesema kuwa wengi waliokufa walikosa hewa kutokana na gesi zenye sumu.
Vyombo vya habari vinaarifu kuwa wengi wa wagonjwa waliokuwa katika  gorofa ya juu ya jumba hilo walishindwa kujiokoa kwa sababu vyumba vyao vilikuwa vimejaa moshi uliotokana na moto huo.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo Lee Hyung Seok ameomba msamaha na kuwaambia wanahabari kuwa  ametenda dhambi kubwa, na kuwa hawezi  kutoa  sababu wakati watu wameaga dunia.
Ajali hiyo ya hospitali  imetokea siku moja tu baada ya watu 7 kuuwawa na wengine 20 kujeruhiwa katika mkasa wa moto uliozuka katika kituo cha mabasi jijini Goyang nchini humo

Maafisa wakuu wa mahakama na usalama nchini Kenya watakutana kwa siku mbili wiki hii kujadili hali ya usalama nchini humo.
Mkutano huo unajiri siku chache baada ya Naibu Rais William Ruto kulalamika kwamba mahakama inarudisha nyuma juhudi za kuwachukulia hatua washukiwa wa ugaidi wanaokamatwa na polisi.
Mkutano huu utakaohusisha maafisa wakuu wa mahakama na usalama nchini Kenya umepangwa kufanyika siku ya alhamisi na ijumaa katika Taasisi ya mafunzo kuhusu mahakama (JTI) .
Jaji Mkuu Willy Mutunga  baada ya kukutana na maafisa wakuu wa usalama katika mahakama kuu alisema kuwa mkutano huo wa siku mbili utafanywa kwa kuzingatia muktadha wa katiba na sheria za kimataifa kuhusu haki za kibinadamu.
Hata hivyo mahakama ilisisitiza kwamba mkutano huo unalenga kujadili sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu na vita dhidi ya ugaidi zinavyokinzana,na kuonyesha kwamba zinapaswa kutumiwa kama zinavyofafanuliwa katika katiba.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini Sudan Kusini  kuhakikisha inatimiza kazi zake  zinazolenga kulinda raia na kusaidia utekelezwaji wa kusitishwa mapambano nchini humo.
Katika azimio lililopitishwa kwa pamoja, nchi 15 wajumbe wa baraza hilo ziliidhinisha makubaliano ya usitishwaji wa uadui yaliyosainiwa Januari pamoja na makubaliano mapya ya kusitisha mapambano yaliyosainiwa mwezi huu na pande mbili zenye mgogoro nchini Sudan Kusini.
Wakati likiongeza muda wa kazi za tume hiyo hadi Novemba 30 mwaka huu, baraza hilo limeeleza kuwa lipo tayari kuzingatia hatua zote sahihi dhidi ya wale waliofanya vitendo vya kuhatarisha amani, utulivu na usalama nchini Sudan Kusini.

Comments