MHE. AZIZ ABOOD KUMSOMEA HITIMA MTOTO NASRA JUMAMOSI HII UWANJA WA JAMAHURI.

              Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Aziz Abood 
Abood
Kaimu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ally Omar akihojiwa na Mtandao huu muda mfupi uliopita.
Na DustanShekidele, Morogoro.
MBUNGE wa Jimbo la Morooro Mjini (CCM) Aziz Abood amejitolea kumsomea hitima marehemu Nasra Mvungi Jumamosi ya wiki hii.

Akizungumza na Mtandao huu kwenye mahojiano maarumu muda mfupi uliopita Kaimu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ally Omar amethibitisha kufanya kikao na katibu wa mbunge huyo.

"Nikweli Leo asubuhi katibu wa Mbunge Bw Mourice Masala alifika ofisini kwangu akidai kwamba Abood anataka kubeba jukumu la kumfanya hitima Nasra hivyo tumekubalina shuhuli hiyo ifanyike jumamosi ya wiki hii majira ya saa 7 mchana pele pele kwenye uwanja wa Jamhuri"alisema Sheikh Omar.

Comments