MHE. ZITTO KABWE AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI. MWILI WASAFIRISHWA KWENDA KIGOMA KWA MAZISHI.

Mama Mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, Bi. Shida Salum enzi za uhai.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mama Mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, Bi. Shida Salum wakati alipokuwa amelazwa ICU katika Hospitali ya AMI jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Zitto Kabwe akiwa na mama yake Shida Salum enzi za uhai wake.
MAMA mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, Bi. Shida Salum amefariki dunia akiwa katika Hospitali ya AMI jijini Dar es Salaam!
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe akiwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wakati wa kuuaga mwili wa mama yake kipenzi Bi. Shida Salum aliyefariki leo kabla ya kusafirishwa kwenda Kigoma kwa mazishi.
Waheshimiwa wabunge na baadhi ya viongozi wakibeba jeneza lililobeba mwili wa marehemu mama yake Zitto Kabwe, Bi. Shida Salum kuingiza kwenye ndege tayari kwa safari ya kwenda Kigoma kwenye mazishi.
Ndege ikiandaliwa ili kuweza kuingiza mwili wa marehemu mama yake Zitto Kabwe.
Prof. Ibrahim Lipumba akijadili jambo na mwenzie baada ya kupakia mwili wa marehemu kwenye ndege kuelekea kigoma kwenye maziko.

Comments