MWENYEKITI WA TAWI LA YANGA MORO AFA KWA AJALI JANA USIKU.

 Injinia Hamis Katoto enzi za Uhai wake aki
hojiwa na Mtandao huu.
                   Kikosi cha yanga
  Picha hii imepigwa muda mfupi uliopita kuonyeha hali iliyo kwa sasa kwenye tawi hilo la Yanga
 Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa mama mzazi wa marehemu Katoto maeneo ya Mji Mpya, eneo ambalo msiba huo upo


                          
 NA DUSTAN SHEKIDELE,MOROGORO.
MWENYEKITI wa tawi la yanga mkoa wa Morogoro lnjinia Hamis Katoto jana majira ya saa 6 usiku akiendesha gari lake GX 100 alipata ajari eneo la Kihonda jirani na Klabu ya Polster na kufariki dunia papo hapo.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi muda mfupi uliopita Mwekahazina mkuu wa tawi hilo Bi,Emmy Kiula alithibitisha mwenyekiti wake huyo kufa kwenye ajari hiyo.

" Nikweli mwenyekiti wetu amefa kwenye ajari jana usiku na kwetu sisi wana yanga hasa wa tawili hili ni pigo kubwa sana,  tumewasilina na familia maziko yatakuwa kesho kwa sasa viongozi wote wa tawi tumepeana majuku ya kufanikisha maziko ya kiongozi wetu"alisema Bi Emmy Kiula ambaye ni diwani mstaafu wa kata ya Mji Mpya mwenye uzalendo mkubwa na timu yake ya Yanga kwa kutoa jengo lake kupakwa rangi za yanga sambamba na kutoa ofisi kwa tawi  hilo.

Mtandao huu ulifika nyumbani kwa mama mzazi wa marehemu eneo hilo hilo la Mji Mpya ulipo msiba huo ambapo dada wa maremu Bi Adha Ponda alithibitisha kaka yake kufa kwenye ajari.

" Nikweli Shekidele rafiki yako lnjini jana usiku kaja kumsalimia mama majira ya saa tatu na kwamba wakati akireje nyumbani kwake Kihonda alipata ajari na kufa papo hapo''alisema Adha na kuangua kilio.

Marehemu Katoto enzi za uhai wake alikuwa lnjini wa barabara halmashauri ya Morogoro Vijijini'DED' ambapo ameliongoza tawi hilo la Yanga kwa zaidi ya miaka 3 kwa mafanikio makubwa.

Kama kawaida mtandao huu utakujuza kila kinachoendelea kwenye msiba huo wa kiongozi wa timu hiyo kubwa hapa nchini

"BWANA AMETOA NA BWANA AMETWA JINA LAKE LIBARIKIWE AMEN''

Habari na Shekidele Blog

Comments