Ney Wa Mitego ni miongoni mwa wasanii waliopata mafanikio makubwa kwenye muziki na kifedha ndani ya mwaka 2013 na 2014. Muziki wake umempa show nyingi na dili za matangazo ambazo hulipa vizuri wasanii.
Kupitia Exclusive interview na sammisago, Ney wa Mitego anasema amehamia kwenye nyumba yake mpya iliyopo maeneo ya Kimara Korogwe na Inathamani ya Pesa za Tanzania Milioni Mia na Themanini.
Ney Wa Mitego anasema alianza kujenga nyumba hii toka mwaka Jana na ni miongoni mwa nyumba zake tatu, mbili bado hazijaisha.
Nyumba nzuri na amejitahidi nampa pongezi. Lakini asidanganye kuhusu gharama. Nyumba ya bati na sio hata ghorofa halafu imejengwa kwa standard ya chini sio kweli kwamba imegharimu milioni 180. Hata ukijumlisha fenicha zake bado haitafika
ReplyDeleteni kweli kabisa wasani kila siku wanapenda kuongeza sana pesa.sijiu kwanini .wanaganya sana tena sana.hiyo nyumba kwa haraka haraka ni kama milioni 80.sasa hivi tumewastukia saana.wawe wanasema ukweli.
ReplyDelete