NGOMA AFRICA BAND AKA FFU KUTUMBUIZA SIKU YA CAMEROON CHALLENGE ,DORTMUND UJERUMANI SIKU YA JUMAMOSI 7, JUNI 2014.
- WAKAMERUNI ZAIDI YA 20,000 USO KWA USO NA FFU-UGHAIBUNI !
Dortmund,Ujeruni, Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka "FFU-Ughaibuni, ukipenda waite viumbe wa ajabu "Anunnaki" au " watoto wa mb..wa" yenye makao kule
ujerumani, bendi hiyo inatarajiwa kutumbuiza katika siku maalumu ya taifa ya kameruni,
katika onyesho la "Cameroon Challenge" siku ya jumamosi kuanzia saa 11 jioni, mjini Dortumund,Ujerumani.
Ngoma Africa band imealikwa na umoja wa wakameruni ughaibuni,ambao ndio wandaaji
wa onyesho hilo la wazi, wakameruni takribani 20,000 waishio ujerumani watachanganyika na wadau wa mataifa mengine kusakata muziki wa Ngoma Africa band,muziki ambao
wapenzi wa bendi hiyo wanaufananisha sawa na gwaride la FFU.
Wasikilize FFU Ughaibuni at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com
Comments
Post a Comment