
Kikosi
cha Taifa Stars ambacho jana (Juni 1 mwaka huu) kiliitupa Zimbabwe
(Mighty Warriors) nje ya michuano ya Afrika baada ya kutoka sare ya
mabao 2-2 kinarejea nchini leo (Juni 2 mwaka huu) kutoka Harare.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itatua Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam saa 12.30
jioni kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea Harare kupitia Nairobi.
Katika
raundi ya pili, Taifa Stars itacheza na Msumbiji ambapo itaanzia
nyumbani kati ya Julai 19 na 20 mwaka huu, wakati mechi ya marudiano
itafanyika Msumbiji kati ya Agosti 2 na 3 mwaka huu.
Wakati
huo huo, Taifa Stars imeendelea kupokea salamu za pongezi kutoka kwa
wadau mbalimbali baada ya kufanikiwa kuvuka kikwazo hicho cha kwanza
katika harakati zake za kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika
mwakani nchini Morocco.
Salamu
hizo zimetoka kwa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Manyara (MARFA), mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akiwakilisha Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA), John Kadutu, na mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ahmed Idd
Mgoyi.
U15 TANZANIA YATUA MEDALI VIFUANI
Timu ya
Tanzania ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 15 iliyoshika nafasi ya
pili katika Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) iliyofanyika Gaborone,
Botswana inawasili leo (Juni 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
U15
ambayo imeshinda mechi tatu, sare moja na kufungwa moja inawasili Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12.30 jioni kwa
ndege ya Kenya Airways ikitokea Gaborone kupitia Nairobi.
Tanzania
ambayo imepata medali za fedha kwa kushika nafasi hiyo ikiwa chini
yaKocha Abel Mtweve ilizifunga Afrika Kusini 2-0, Botswana 2-0,
Swaziland 3-0 na ikatoka sare ya bao 1-1 na Mali. Ilifungwa mabao 2-0 na
Nigeria ambao ndiyo walioibuka mabingwa.
Wachezaji
16 waliounda kikosi cha Tanzania ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos
Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove
Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka,
Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Comments
Post a Comment