
Mkurugenzi
Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez (wa pili kulia) akipongezana na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) Engineer George
Mulamula mara baada ya kutiliana saini ya ushirikiano ambapo Tigo
itawawezesha washiriki wa teknohama wa DTBi kuendeleza vipaji vyao
kupitia mpango maalum wa mafunzo na biashara ambayo itasaidia kukuza
ajira nchini kupitia taaluma ya teknohama. Kushoto ni Waziri wa Sayansi,
Mawasiliano na Teknolojia Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Hassan Mshinda.

Mkurugenzi
Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez (kulia) akitiliana saini na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) Eng. George
Mulamula kama ishara ya ushirikiano kati ya Tigo na kituo hicho cha
biashara ya teknohama DTBi. Wanaoshuhudia kutoka nyuma ni Waziri wa
Mawasiliano na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (kushoto) na
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dk. Hassan Mshinda. Tigo itatoa nafasi ya
kuwasomesha watanzania 10 katika ngazi ya Shahada ya Uzamili kila mwaka.

Waziri
wa Mawasiliano na Teknolojia Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (katikati) na
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez (kushoto) wakimsikiliza kwa
makini mmoja wa washiriki wa mpango maalum wa Tigo na DTBi katika
kukuza vipaji vya teknohama Bw. Godfrey Magila ambaye ameweza kubuni
programu ya kuangalia vipindi vya Bunge kupitia simu za mkononi za
kisasa. Tigo pia itatoa fursa za mafunzo kwa vitendo na nafasi za ajira
kwa wale ambao wamejikita katika masomo ya Teknohama.
Waziri
wa Mawasiliano na Teknolojia Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani)
wakati wa hafla fupi ya utiliaji saini kati ya kampuni ya Tigo na kituo
cha biashara ya teknohama DTBi. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw.
Diego Gutierrez na Afisa Mtendaji Mkuu wa DTBi Eng. George Mulamula

Afisa
Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) Engineer
George Mulamula akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa
(hawapo pichani)
wakati wa hafla fupi ya utiliaji saini kati ya kampuni ya Tigo na kituo
cha biashara ya teknohama DTBi.
Chanzo : Mtaa Kwa Mtaa Blog
Comments
Post a Comment