ALLY KIBA IS BACK SIKILIZA NYIMBO ZAKE HAPA [AUDIO].

Najua mashabiki walikua wanaisubiria sana hii post ambapo good news zaidi ni kwamba Ali Kiba ameachia single mbili mpya kwa wakati mmoja na moja inaitwa “Mwana” na nyingine “Kimasomaso”.
Tunamfahamu staa huyu kama mkali wa hit single kama Cinderella, Mapenzi yanarun dunia, Single boy, na Dushelele lakini unaambiwa Cinderela ndio wimbo mwingine ambao mpaka sasa una rekodi ya kuuza copy nyingi Afrika Mashariki mwaka 2008.
Sehemu ya mafanikio yake mengine ni pamoja na kushinda tuzo mwaka 2012 best Rhumba/ Zouk ya “Dushelele” kwenye tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards. (KTMA).
Kuhusu hizi nyimbo mbili mpya, unaweza kuzisikiliza kwa kudownload bure na kwa njia rahisi kupitia  www.mkito.com.



Comments

  1. Mwana ni balaa...du nimeupenda sana huu wimbo....mashairi yake sasa ukiyasikia kwa kina duh mazuri sana

    ReplyDelete

Post a Comment