ASKARI FEKI ALIYENASWA CHAMAZI JUMAMOSI ILIYOPITWA AONYESHWA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI.

Kamishna Kova (katikati) akionesha kidole kwa polisi feki aliyekamatwa.
Sura ya ‘karibu’ ya askari huyo feki aliyekamatwa aitwaye Robson Seif Mwakyusa (30).
Kova akionyesha baadhi ya sare za jeshi la polisi alizokamatwa nazo polisi huyo feki.
Waandishi wa habari waliokuwa katika tukio hilo.
JESHI la Polisi Kanda ya Dar es Salaam linamshikilia na kumhoji mtu mmoja anayeitwa Robson Seif Mwakyusa (30) mkazi wa Kijitonyama Jijini Dar, kwa tuhuma za kujifanya ofisa wa polisi kikosi cha usalama barabarani  huku akifanya ukaguzi wa makosa ya usalama barabarani
Mtuhumiwa huyu alikamatwa umamosi  iliyopita huko Kata ya Chamazi, Mbagala-Majimatitu Mkoa wa Kipolisi Temeke akiwa amevalia sare za polisi na cheo cha stesheni sajenti na akiwa na leseni mbalinbali za magari, ‘radio-call’, stakabadhi, na vitu vingine.
Video ya tukio hili itakuja hivi punde.
(Na Gabriel Ng’osha/GPL)

HAPA CHINI NI PICHA ZA AWALI WAKATI AKIKAMATWA 
 Askari feki wa Usalama Barabarani ambae Jina lake halikufahamika haraka akiwa chini ya Ulinzi mkali wa Askari Polisi (hayupo pichani) mara baada ya kukamatwa kwa kujifanya ni askari wa usalama barabarani huku akifahamu kuwa ni kosa kisheria. Inasemekana Mtuhumiwa aliwahi kuwa askari wa Usalama barabarani ambapo kituo chake cha Kazi kilikuwa Mkoa wa Pwani na ni mmoja kati ya askari waliofukuzwa kazi kwa kuenda kinyume na taratibu na sheria za Jeshi la Polisi Tanzania
 Askari Polisi ambae jina lake halikufahamika mara moja (Mwenye sweta) akimkamata kwa makini mtuhumiwa aliyejifanya askari wa usalama barabarani leo katika eneo la Chamazi Jijini Dar Es Salaam
Askari feki akishangaa na kuduwaa mara baada ya jeshi la Polisi Kumtia nguvuni leo Katika Eneo la Chamazi Jijini Dar Es Salaam Mapema leo. Picha Kwa Hisani ya Mdau.

Comments