Kampuni ya Apple imezindua saa ya kisasa - the Apple Watch - ambayo ni bidhaa yake mpya tangu iPad ya kwanza na tangu kifo cha mmoja wa waasisi wake Steve Jobs.
Kifaa hicho huendesha programu tumishi (apps) na pia hufuatilia mienendo ya kiafya na vilevile huwasiliana na iPhone.
Wakati wapinzani wa Apple tayari wana saa za mtindo huo, wataalam wanasema Apple ina historia ya kuchelewa kuleta bidhaa zake sokoni lakini hubadili kabisa mwelekeo wake.
Apple pia imezindua simu aina mbili ambazo ni kubwa kuliko za zamani.
iPhone 6 ina skrini yenye ukubwa wa sentimita 11.9 na iPhone 6 Plus skrini yake ina ukubwa wa sentimita 14.0, mabadiliko ambayo wachambuzi wanasema yatazuia wateja kuhamia simu za Android.
Apple vilevile imetangaza huduma mpya ya malipo ijulikanayo kama 'Apple Pay' ambayo mkurugenzi mkuu Tim Cook amesema ana imani "itachukua nafasi ya pochi".
Comments
Post a Comment