Watu wanne - Watanzania wawili na Wanyarwanda wawili- waliokutwa na hatia ya kutaka kumuua mkosoaji wa Rais wa Rwanda Paul Kagame nchini Afrika Kusini wamehukumiwa kwenda jela kwa miaka minane kila mmoja. Mkuu wa zamani wa jeshi la Rwanda Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa alinusurika jaribio hilo karibu na nyumbani wake jijini Johannesburg mwaka 2010. Rwanda imekuwa ikikanusha kuhusika na tukio hilo. Waendesha mashtaka awali walitaka adhabu ya miaka kumi na mitano. Jaji Stanley Mkhari amesema watu hao hawakuwa wahusika wakuu, bali walikodishwa kufanya hivyo.
Comments
Post a Comment