SIKILIZA HEKAHEKA YA CLOUDS FM INAYOHUSU MAUAJI YA JACKY NA WANZE

Kwenye Leo Tena ya Clouds FM, Hekaheka ilikuwa inahusu tukio la wasichana wawili marafiki ambao miili yao iliokotwa baada ya kuuawa, ambapo ndugu wa karibu wa msichana mmoja wamesema wanahisi tukio hilo limetokana na urafiki ulioanzishwa kupitia Facebook kati ya wasichana hao.
Urafiki wao umedumu kwa muda wa kipindi cha miezi mitatu na siku ambayo inasemekana walitekwa, mmoja wa wasichana hao ambaye anaitwa Jacky alimwomba rafiki yake huyo ambaye anaitwa Wanze waende Mlimani City.
Mama wa Wanze amesema alipigiwa simu na mdogo wake kumpa taarifa kwamba Wanze alimtumia taarifa kuwa ametekwa siku tatu zilizopita, lakini mdogo wake huyo alisita kumpa taarifa hizo kwa kuwa alihisi hakuna ukweli mpaka siku ambayo alipigiwa simu na kaka yake aliyekuwa safarini kuja Dar na kumtaarifu juu ya msiba wa mtoto wao.
Baada ya kupata taarifa hizo waliamua kumtafuta Jacky ambaye wao walikuwa wanamfahamu kwa jina la Salha ambapo muda mfupi baadaye wakapata picha za Salhaambaye pia alikuwa amefariki.
Mazingira ya kifo cha wasichana hao inaonekana waliteswa kwa kunyongwa kamba mpaka kufariki.
Unaweza kubonyeza play hapa kuisikiliza Hekaheka hiyo.



Credit; Millardayo.com

Comments