Uhuru Kenyatta afutiwa mashtaka na ICC

Mwendesha mkuu wa mashtaka, Fatou Bensouda ameondoa kesi dhidi ya Rais huyo wa Kenya akidaiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007/2008. Mahakama ilikuwa imempa Bensouda wiki moja kuamua ikiwa ataendelea na kesi dhidi ya Kenyatta au la. Kenyatta alishtakiwa kama mshukiwa mkuu wa ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/2008 akituhimiwa pamoja na William Ruto ambaye ni Naibu Rais.

Comments